Mawakili wapambana vikali kielelezo cha barua kesi ya kina Mbowe

Muktasari:

  • Mawakili wa utetezi na Serikali katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo Ijumaa Novemba 26, 2021 wamepambana vikali kuhusu ombi la mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Mohamed Ling’wenya kutaka mahakama ipokee barua walioliandikia Jeshi la Polisi kutaka uthibitisho wa kituo alichokuwa akifanyia kazi mwaka 2020 shahidi wa Serikali, askari mpelelezi, Ricardo Msemwa.



Dar es Salaam. Mawakili wa utetezi na Serikali katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo Ijumaa Novemba 26, 2021 wamepambana vikali kuhusu ombi la mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Mohamed Ling’wenya kutaka mahakama ipokee barua walioliandikia Jeshi la Polisi kutaka uthibitisho wa kituo alichokuwa akifanyia kazi mwaka 2020 shahidi wa Serikali, askari mpelelezi, Ricardo Msemwa.

Mabishano hayo yamekuja baada ya Ling’wenya kuibua hoja hiyo jana Alhamisi dhidi ya shahidi huyo wa pili wa Serikali katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayohusu uhalali wa maelezo ya onyo ya mshtakiwa huyo.

Ling'wenya ambaye jana alianza kutoa ushahidi wake wa utetezi, akiwa ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ndogo, ameliandikia barua Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala kulitaka liwasilishe vielelezo vya kuthibitisha ni wapi shahidi hyo wa serikali alikuwa akifanya kazi mwaka 2020.

Vielelezo anavyoviomba ni pamoja na amri ya shahidi huyo kuhama kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Kitabu cha Matukio (OB) na kitabu cha kusaini kuonesha uwepo wa ofisa eneo la kazi.

Hivyo, aliomba barua hiyo ipokewe mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi wake na iwe kielelezo cha ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi hiyo ndogo.

Ling'wenya amefikia  hatua hiyo kupinga maelezo ya Msemwa kuwa mwaka 2020 alikuwa akifanya kazi Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam na kwamba alimpokea mshtakiwa huyo kituoni hapo Agosti 7, 2020 na kuingiza jina lake katika Kitabu cha kumbukumbu za mahabusu kabla ya kuhamishiwa Kituo cha Polisi, Oysterbay.

Ifuatayo ni sehemu ya maelezo ya mawakili wa pande zote wakiwasilisha hoja kuhusu kielelezo hicho.

Wakili Chavula: Mheshimiwa jaji kwenye hoja ya chain of custody ni mtizamo wetu katika eneo hili shahidi ameshindwa kuitengeneza kabla sijaendelea naomba kielelezo.

Wakili Chavula: Hoja yetu katika eneo hili iko katika maeno mawaili.

Eneo la kwanza shahidi ameieleza mahakama kuoneshwa barua hii na la pili shahidi alisema alimpa maelekezo wakili wake Fredrick aandike barua hii, lakini barua hi inaonekana ineandikwa na  Peter Kibatala.

Mahakama haijaelezwa barua hii imetoka vipi kwa Wakili Kibatala na kumfikia shahidi.

Katika mazingira yaliyopo msingi uliowekwa na shahidi labda wakili Peter Kibatala aende pale akatoe ushahidi wake wa namna barua hii ilivyotembea mpaka kufika kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala na kurejeshwa hapa mahakamani kwa ajili ya kutolewa kama kielelezo, walau hapo unaweza kusema chain imekuwa sawa

Wakili Chavula: Lakini kwa hali ilivyo hata yeye mwenyewe hawezi kwenda hapo kutoa ushahidi. Kwa hiyo mnyororo wa uhifadhi wa nyaraka hii kuanzia ilipopokelewa kwa Kamanda wa Polisi Ilala mpaka kumfikia shahidi Jana, mwenzetu Matata (wakili wa Ling'wenya) amewshindwa kumuongoza shahidi huyu.

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji, Kama tulivyokwishazungumza jana tunarejea tena kielelezo hiki sicho ambacho shahidi anataka kukitoa.

Wakili Chavula: Shahidi anataka kutoa barua aliyompelekea Kamanda wa Polisi Ilala. Barua anayotaka kutoa ina mhuri wa Mahakama Kuu Divisheni, lakini anayotaka kuitoa ina mhuri wa High Court of Tanzania Corruption and Economic Division, hivi ni vitu viwili tofauti.

Wakili Chavula: Nasi tunasema ule mnyororo uliohifadhi kwa hali umekatika, pasipo kuwa na maelezo kama ilivyo hapa mnyororo wa uhifadhi umekatika na kukatika kwa mnyororo wa uhifadhi kunaaathiri authenticity ya kielelezo hiki. Hilo ni eneo la kwanza la chain of custody.

Wakili Chavula: Eneo la pili nyaraka hii ni nakala iliyopelekwa kwa Mheshimiwa Msajili wa Mahakama. haijaelezwa ushahidi mbele ya Mahakama yako kuwa ni nani haswa alikabidhiwa nyaraka hii na msajili baada ya ku- acknowledge kupokea na huyo alokabidhiwa nyaraka hii ni Mheshimiwa Naibu Msajili aliifikisha kwa namna gani kwa shahidi.

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji katika hatua hi mahakama yako ilipaswa ipatiwe ushahidi na shahidi kuonesha kielelezo hicho baada ya kutoka kwa Msajili kilimfikiaje

Wakili Chavula: Kwa hiyo hata kama mahakama ikisema hiki kielelezo ndicho kilichopokewa kwa Kamanda bado kina mapungufu.

Wakili Chavula: Kwa hoja hizo tunaiomba mahakama yako isipokee kielelezo hiki. Kwa sababu misingi ya uhifadhi wa kielelezo hiki kuanzia ilikotoka kwa Mheshimiwa Naibu Msajili mpaka kumfikia shahidi hapa mahakamani siku ya jana na hivyo hivyo misingi ya uhifadhi wa kielelezo hiki kutoka kwa Kamanda wa Ilala mpaka kumfikia shahidi huyu siku ya jana haijawekwa wazi.

Wakili Chavula: Tunatambua kisheria chain of custody haiwezi iuwa established na shahidi na Mahakama ita- determine mwisho wa shauri, lakini haina maana kwamba wakati shahidi anatoa ushahidi asiieleze mahakama namna kielelezo hicho kilivyofika mikononi mwake

Wakili Chavula: Katika kuunga mkono tunaielekeza mahakama yako katika shauri la DPP vs Sharif Mohamed Athuman na wenzake sita, ambalo siku ya jana tuliielekeza hapa kuanzia ukurasa wa nane mpaka wa 10.

Wakili Chavula: Hivyo kwa hoja hizo tunaiomba mahakama yako isipokee kielelezo hiki

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji Naomba nielekee kwenye eneo la relevance.

Wakili Chavula: Moja ya vigezo vya kupokea kielelezo no relevance. Tunairejesha tena mahakama yako kwenye shauri la DPP vs Sharifu Mohamed ukurasa wa saba aya ya tatu

Wakili Chavula: Mahakama ikisema kigezo hiki cha relevance kinatuma hata kwenye shauri dogo.

Wakili Chavula: Shauri hili dogo lililoko mbele yako linamhusu Mohamed Abdillahi Ling'wenya dhidi yetu sisi Jamhuri na dhidi ya mshtakiwa wa kwanza, wa pili na wa nne.

Wakili Chavula: Barua hii kwa namna ilivyo na kwa namna ilivyoandikwa inamhusu Freeman Mbowe.

Wakili Chavula: Na hata aliyeandika amebainisha anamwakilisha Freeman Aikael Mbowe.

Wakili John Mallya anapinga kuwa anachofanya wakili ya kuingia kwenye maudhui ya kielelezo ni kinyume.

Wakili Chavula: Mshemiwa Jaji tunachozungumza ni relevance, hakuna namna ya kuzungumza relevance bila kuangalia kielelezo, mbona hawakupinga nilivyosema imeandikwa na Kibatala?

Wakili Chavula: Katika mazingira haya unakwepaje kuzungumza yaliyomo ndani?

Wakili Chavula: Sisi tunataka tuoneshe utofauti alichozungumza jana shahidi na kilichopo.

Wakili Kibatala anachofanya wakili ni out of context na Mahakama yako ilishatoa ruling lakini kila mara wenzetu wanajaribu kubadilisha uamuzi wa Mahakama.

Wakili Mtobesya: Hicho kifungu cha saba akichokizungumza wakili kinahusu ushahidi uliopo na sisi ndio tunajaribu kuingiza ushahidi.

Jaji: Umeelewa hoja yao?

Wakili Chavula: Nimeelewa Sana

Jaji: Unahisi hawana hoja?

Wakili Chavula: Hawana kabisa. Mheshimiwa Jaji kifungu hiki (cha 7 cha Sheria ya Ushahidi) kina control kuingiza ushahidi bila utaratibu kinadhibiti kuingiza takataka. Na sisi tunazungumza ushahidi na namna ya kuingiza, sasa sijui hawa wenzetu wanazungumza nini hawa?

Mallya: Mshemiwa Jaji sisi hatumzuii kuzungumza relevance ila kuingia kwenye kielelezo.

Jaji Tiganga: Naomba nitoe uamuzi. Mahakama ilishatoa maelekezo kuwa unapotaka kuzungumza relevance ya kielelezo hakuna namna utaacha kukirejea isipokuwa content. Namna unavyotaka kufanya Chavula unataka kuingia ndani zaidi kwenye kielelezo. Na Mimi nimeshakurekodi kwa hiyo unataka kufanya marudio

Wakili Chavula: Mheshimiwa kielelezo hiki siyo relevance. Kwa kuwa ushahidi alioutoa awali unakinzana na anachotaka kukitoa ni maoni yetu kielelezo hiki sio relevant. Kilichoko mbele yako ni mshtakiwa wa nne kuandika barua kwenda kwa Kamanda wa Polisi Ilala.

Jaji: Mshtakiwa wa nne!

Wakili Chavula: Shahidi, ama mahtakiwa wa nne sorry wa tatu.

Wakili Chavula: Kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha Sheria ya Ushahidi tulitarajia alete ushahidi wa kile alichokizungumza lakini sicho alichokileta hapa.

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji Naomba tuelekee kwenye hoja yetu ya foundation. Ili kielelezo kiweze kupokelewa, ni lazima msingi ama foundation ya ushahidi huo ujengwe. Tukirejea ushahidi uliotolewa na shahidi siku ya jana wa kumpa maelekezo Wakili Fred na kuoneshwa kielelezo ni maoni yetu wenzetu wameshindwa kujenga foundation.

Mheshimiwa Jaji, Kama tulivyoielezea mahakama awali chanzo cha nyaraka hii si yeye wala si Wakili wake.

Wakili Chavula: Chanzo cha nyaraka hii ni adverse party kwenye kesi hii ambaye mwisho wa siku kama kitapokewa atafanya cross examination

Wakili Kibatala anapinga kuwa wakili Chavula anasababisha point of interest tunaomba sana asiende huko

Chavula: Mheshimiwa wenzetu sijui kwa nini wanayaogopa haya maana wao ndio wanayaleta, na waliyaleta wakijua kuwa mwisho wa siku hatakuwa hivi. Kwa hiyo wavumilie tu.

Jaji: Haya Sasa jibu hoja.

Chavula: Mheshimiwa Jaji sisi tuko sahihi, sahihi kabisa lakini kwa kukupunguzia mzigb wa kuandika ruling tuanaachana nayo.

Jaji: Nashukru kwa kunipunguzia mzigo.

Wakili Chavula: Anaendelea. Mheshimiwa Jaji tunairejesha mahakama yako kwenye shauri la DPP VS Sharif Mohamed kuanzia ukurasa wa nne mpaka wa saba ambapo mahakama ilisema ili ku-meet test ya liability ni lazima foundation iwe imejengwa na kushindwa kujenga foundation athari yake inakwenda kuathiri competence ya kielelezo

Wakili Chavula: Sasa ameshindwa kujenga foundation hivyo tunaomba mahakama isipokee barua hi kwa sababu barua hii ni incompetent.

Mheshimiwa Jaji Naomba nimwachie mwenzangu Pius Hilla amalizie.

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji nianze kwa kusema kwamba naunga mkono mawasilisho ya mwenzangu Chavula lakini pia niongeze kidogo.

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji shahidi aliyeko kizimbani ameshindwa ku-authenticate kielelezo. Authentication ilitakiwa ifanyike kabla ya kuomba kielelezo kwa mujibu wa shauri la DPP dhid ya Sharifu authentication ni suala la msingi.

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Alipooneshwa barua akaesma atatambua kwa signature ya wakili Kibatala lakini hakusema ana utaalamu gani na signature ya Kibatala na ameifahamu lini na vipi.

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Lakini pia hakuweza ku-authenticate kwa kueleza unique features, hakutaja reference number ya  barua hiyo.

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Kitu pekee alichokitaja kuitambua ni kwamba kuna jina lake.

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji kwa mazingira ya barua hi jina lake pekee  halitoshi ku-authenticate maana yeye si mwandishi wa barua, alichokifanya ni kumuelezea wakili Fred (aandike barua).

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Lakini pia jina pekee halitoshi kwa sababu hakuna ushahidi kuwa alijiridhisha kuwa alichokiandika Kibatala ndicho alichomweleza wakili Fred.

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji jina pekee halitoshi maana hajasema barua hii ilimfikiaje.

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Kwa hiyo Mheshimiwa katika mazingira hayo shahidi mwenye ni incompetent na kielelezo chenyewe ni incompetent.

Hilla: Mheshimiwa Jaji Wakili Chavula ameeleza vizuri suala la chain of custody. Hata mbali na document maelezo pekee pia haya-apply.

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Shahidi kasema barua aliyo-instruct iandikwe ni kwenda kwa RPC Ilala lakini hata assurance yenyewe ya barua hiyo haipo.

Wakili Kibatala; Mheshimiwa samahani kabla hajasimama Wakili Hilla ulitoa maelekezo fulani kuhusu kurudia uliyoongelea sijui ilikuwa no off record au vipi?

Jaji: Ilikuwa off record

Kibatala: Basi naomba utoe maelekezo tena maana naoma kama mwenzetu anarudia siyo anajirudi bali anarudia kile kilichokwishasemwa.

Jaji: Maelekezo japo yalikuwa off record lakini bado ndio mwongozo. Tunatarajia submission yako haitakuwa ndefu maana mengi yameshazungumzwa.

Hilla: Mheshimiwa mimi nazungumzia assurance ambayo mwenzagu Chavula hajaizungumzia. Shahidi alipaswa atoe assurance kwamba alichokielekeza kiandikwe ndicho kilichoandikwa.

Akirejea amri za Magereza, baada ya kuzisoma wakili Hilla anaeleza kuwa kwa mujibu wa amri hizo za Magereza shahidi mawasiliano yoyote yalipaswa yapitie kwa Afisa wa Magereza Mfawidhi, lakini hakuna ushahidi kuwa nyaraka hii ilipitia kwa Afisa wa Magereza aliko. Maana yake ni kwamba reliability ya nyaraka Mheshimiwa siyo authentic na kwa kuwa siyo authentic haijafuata utaratibu huo inapaswa isipokewe.

Hilla: Hi ni mahakama ya sheria haiwezi kupokea nyaraka ambazo zinakuja bila utaratibu.

Hilla: Kwa mazingira ya shauri hii huyu kwa kuwa ni mahabusu yuko chini ya uangalizi wa Magereza, nyaraka hii imepatikana kinyemela na haikufuata utaratibu.

Hilla: Mheshimiwa Jaji kwa hayo machache naomba kuishia hapo nisiichoshe mahakama.

Hilla: Wenzangu wameniambia hawana cha kuongeza basi naomba mahakama ikubaliane na pingamizi letu ione kuwa shahidi na siyo competent, kielelezo siyo relevant na hakuna foundation iliyojengwa.

Baada ya upande wa mashtaka kumaliza hoja zao, sasa mawakili wa utetezi nao wanajibu hoja

Anaanza wakili Jeremiah Mtobesya anayemtetea mshtakiwa wa kwanza Halfan Bwire Hassan

Wakili Jeremiah Mtobesya: Kama tulivyosema Jana tunaunga mkono maombi ya shahidi aliyeko kizimbani ya kutaka kupokea kielelezo.

Wakili Jeremiah Mtobesya: Mahakama ya Rufani ilishasema kuwa katka kupokea kielelezo lazima iangalie competence ya shahidi na kielelezo chenyewe, relevance na foundation.

Wakili Jeremiah Mtobesya: Kwa maoni yetu shahidi huyu pamoja na kielelezo ni competent kwa kuwa amekidhi vigezo hivyo.

Wakili Chavula anasimama na kupinga kuwa hakuna utaratibu wa kukubali kupokea kielelezo na kutoa sababu na anaomba mwongozo.

Mtobesya naye anaomba mwongozo kuwa ni vipi atatoa sababu zake kama ni kimyakimya au namna gani.

Jaji Tiganga: Kidando (Wakili wa Serikali) kabla ya hapa tuliongea kule ndani.

Wakili Kidando: Ni kweli Mheshimiwa Jaji tuliongea kwamba wanaweza kutoa sababu na hivyo tunaomba watoe sababu tu na si kufanya submission.

Jaji Tiganga: Mtobesya, ni kweli nilikubali kutoa sababu, lakini huna haki ya kufanya submission na kujibu hoja za upande wa mashtaka, kwa hiyo unaweza kujikita tu kwenye kielelezo hicho.

Wakili Mtobesya: Ni sawa Mheshimiwa Jaji lakini sasa napata tabu namna gani nitamtetea. Basi labda niombe pale ambapo nitakuwa nakwenda nje basi uwe unaniongoza.


Mtobesya anaendelea na anasema kuwa anakubaliana na kielezo hicho kwa sababu shahidi ni competent.

Wakili Chavula anasimama tena na kupinga akisema kuwa atoe sababu tu na asijibu hoja maana kusema kuwa shahidi ni competent kwa sababu ameeleza kwenye ushahidi wake ni kujibu hoja zao.

Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji uliomsimamisha Kidando nilijua utanisimamisha na mimi. Haya masuala tulishayaongea kwenye briefing lakini kwa sababu wakili Chavula hakuwepo ndio maana anataka kutuletea kanuni zake, na naona Kidando kama ameyakana.

Jaji: Lakini hajayakana huo ni mtizamo wako. Hapa napata tabu kwamba tunazungumzia haki za watu si za washtakiwa bali pande zote.

Jaji: Katika hili ninyi nyote mko upande mmoja na upande wa mashtaka na mko upande tofauti na mshtakiw wa pili na wa tatu na wa nne.

Kwa hiyo ninyi mahakama jana ilisema mtatoa tu sababu lakini si kwa kiwa kiwango cha kujibu hoja za upande wa mashtaka maana wao hawatapata nafasi ya kujibu hoja zenu.

Jaji: Hi kesi ni ya mshtakiwa wa tatu, ndio anapaswa kujibu hoja kwa hiyo ninyi jibuni lakini si kwa namna ambayo itaingilia haki za upande mwingine.

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji napata tabu namna gani nitoe sababu bila kutoa hoja vipi Kama ningekuwa napinga?

Jaji: Ungeweza kutoa hoja lakini si kwa kiwango cha kuingilia haki za upande wa pili.

Wakili Chavula anasimama na kusisitiza kuwa hawana mawakili wa washtakiwa wengine hawana haki ya kutoa hoja na anahoji kama wanakubalia barua hiyo ipokewe wanahofu nini

Wakili Kibatala anasimama huku akionesha kuchukizwa na kauli hizo lakini Jaji anamtaka akae naye anakaa.

Jaji Tiganga: Huyu Mtobesya anasimama kwa sababu anatetea maslahi ya mteja wake, siyo kwamba anapenda tu kuja hapa maana ana kesi nyingine huko Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na kwingineko lakini anakuja hapa kwa kuwa ni mteja wake.

Jaji Tiganga: Hapa ndipo ninapopata shida kwamba ni namna ya kulinda haki za kila upande, ninyi kwa sababu mmekaa huko mnaona ni rahis lakini mimi niliyekaa hapa ndio napata tabu. Kwa hiyo jitabidini kutokuvuka na kuingilia haki za upande mwingine.

Chavula: Basi Mheshimiwa Jaji kwa hayo acha tu watoe hoja zao.

Baada ya maelezo hayo wakili Mtobesya anaendelea.

Wakili Mtobesya anasema anaunga mkono barua hiyo kupokewa kwa sababu shahidi amekidhi vigezo. Amemtambua jina lake, jina la aliyeiandika.

Wakili John Mallya: Nami naunga mkono maombi ya mshatakiwa kuawasilisha barua hiyo ipokewe na nakubaliana na sababu alizozitoa Mtobesya.

Kibatala: Nasi tunaunga mkono maombi ya mshtakiwa kupokea barua hiyo maana alisema anaitambua kwa Mhuri wa Naibu Msajili, alisema ndiye aliyetoa maelekezo kwa wakili wake Fred na kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, kwamba ilielekezwa kwa RPC Ilala, Kwamba alioneshwa na akaitambua, tulimsikkia akitaja vilivyoombwa ikiwemo Removal Order, OB na Statio Diary.

Kibatala: Hivyo kwa sababu hizo sisi tunaunga mkono maombi ya shahidi kupokewa kwa barua hiyo kuwa kielelezo.

Matata: Ni submission yetu kwamba mteja wetu ana haki inayolindwa na Katiba ya Nchi ibara ya 13(6) (b) ambayo si tu anapokuwa mahakamani lakini pia hata anapokwenda gerezani sisi mawakili tuna haki ya kuonana na wateja wetu wakati wowote.

Matata: Mheshimiwa ukisoma Police General Orders zinalenga kudumisha mahusiano kati yao mawakili na wateja wetu na hakuna mahali popote zinazuia.

Matata: Mheshimiwa Jaji wenzetu upande wa pili labda ni kwa sababu hawana wateja magerezani lakini sisi ambao kila mara tunakwenda magerezani utaratibu uliopo ambao unahusisha kumuona bwana Jela na mhuri kugongwa ni wa namna mbili.  

Matata: Ni either mtuhumiwa au mahabusu anapotaka kuandika barua kwenda nje kwa ndugu au kwa Wakili ndipo utahitaji barua hiyo ifike kwa Bwana Jela na igongwe mhuri..

Matata: Namna ya pili ni pale mtu anapotoka nje labda wakili na ana nyaraka anataka kumpelekwa mtuhumiwa kuisaini, hapo  Bwana Jela atahusika kitakachofanyika wataichukua ile nyaraka na watai-type wao, wataipeleka ataisaini mtuhumiwa na kisha watagonga mhuri, kisha wakili atakabidhiwa na ataondoka nayo.

Matata: Mheshimiwa Jaji na nyaraka nyingine ambayo haihitaji kusainiwa na mteja wako, huwa haigogwi mhuri wanachokifanya ni kuichukua na kuikagua kuhakikisha kuwa nyaraka ile iko kisheria

Matata: Hapo ni kuonesha kwamba haina content ambazo zinavunja sheria.

Matata: Mheshimiwa Jaji ni ushahidi wa shahidi aliyeko kizimbani, anasema yeye alioneshwa barua na wakili wake akiwepo na wakili kiongozi wa jopo la utetezi jana hapa.

Matata: Na si  kukaa nayo, alioneshwa tu.

Matata: Mheshimiwa kwa kusema alioneshwa hapa mahakamani, hoja ya kuwa barua ile ilitakiwa kuwa na mhuri na kupitia kwa Bwana Jela inakosa mashiko

Matata: Mheshimiwa Jaji ni submission yetu pia kwamba mteja anapokuwa eneo la mahakama, anakuwa na haki ya kuonana na kuwasiliana na mawakili wake na kinachotakiwa ni kuwaomba Askari Magereza wanaokuwa naye kwa siku hiyo na hiyo haihitaji mpaka twende kwa Bwana Jela.

Matata: Ndio maana wakiwa hapa mahakamani sisi mawakili tunakuwa na haki ya kubadilishana vimemo , wao wanatuandikia na sisi tunawaandikia hatuhitaji kwenda kwa Bwana Jela.

Matata: Mheshimiwa Jaji Ni submission yetu pia kwamba mteja anapokuwa eneo la mahakama, anakuwa na haki ya kuonana na kuwasiliana na mawakili wake na kinachotakiwa ni kuwaomba kwa Askari magereza wanaokuwa naye kwa siku hiyo na hiyo haihitaji mpaka twende kwa Bwana Jela.

Matata: Ndio maana wakiwa hapa mahakamani sisi mawakili tunakuwa na haki ya kubadilishana vimemo, wao wanatuandikia na sisi tunawaandikia hatuhitaji kwenda kwa Bwana Jela.

Matata: Mheshimiwa Jaji jana tulikuwa tunajua upande wa mashtaka wanakuja kuendelea na ushahidi, lakini wakaja na kufunga ushahidi wao. Sasa tunajiuliza angewezaje shahidi kutoa ushahidi wake kabla hatujakaa naye na kumuandaa kutoa ushahidi.

Wakili Matata: Mheshimiwa Jaji ni maoni yetu pingamizi hili halina mashiko kwa sababu haliangukii kwenye test admissibility ambapo zinataka shahidi awe competence, relevant na Materiality

Matata: Kwenye competency shahidi na barua aliyotaka ni competent kwa kuwa yeye ndio aliyetoa maelekezo kwa Wakili wake Fredrick na Peter Kibatala.

Matata: Maelekezo hayo aliyatoa baada shahidi Msemwa kumaliza kutoa ushahidi wake akidai washtakiwa baada ya kukamatwa Moshi walipelekwa Central Polisi kitu ambacho shahidi hakubalini nacho

Matata: Alitoa maelekezo barua iende kwa RPC Ilala akitaka vitu vitatu remove order, kitabu cha matukio OB, na Station Diary ambayo alifafanua kwa kutumia kifaa kilichopo jeshini kinaitwa roster.

Matata: Wakati anaongozwa kutoa ushahidi aliweza kutaja features na akaweza kuzitaja akataja kesi namba, akataja jina la jopo la mawakili Peter Kibatala pia alitaja jina la shahidi Msemwa pamoja na mhuri.

Matata: Pia wakati shahidi anaongozwa aliweza kutambua subject matter aliweza kuzungumzia remove order, OB na Stationary diary

Matata: Pia nlimuuliza alitambuaje sahihi ya Peter Kibatala ambaye ni kiongozi wa jopo la mawakili akasema anaitambua kwa kuwa ni wakili wao wa muda mrefu toka kisutu na alikuwa akiwaandikia barua mara kwa mara na hata kesi hii ilivyohamishiwa mahakama kuu ameendelea kuwa kiongozi wa jopo la mawakili.

Matata: Pia alitambua jina lake na barua ile imekuwa copy kwake hivyo ni maoni yetu shahidi amekuwa competent.

Matata: Mheshimiwa Jaji kabla hujatoa uwamuzi ujikumbushe uwamuzi ulioutoa hapa mahakamani Novemba 16,2021 wakati maombi yalilietwa na shahidi wa pili katika kesi hii ndogo Msemwa kutoka kwa Naibu Msajili na kuwa copy kwa Msemwa kama ilivyo kwa shahidi huyu maamuzi ya mahakama yalisema mtu akiwa copy hajavunja utaratibu.

Matata:  Barua hii ni relevant kwa sababu zifuatazo.

Shahidi aliieleza ni kwa nini aliomba barua hii iandikwe ili aweze kupewa nyaraka kutoka kwa RPC Ilala ili kuweza kudhibitisha askari Msemwa aliyekuwa shahidi wa pili kwenye kesi hii ndogo alikuwa central Agost 7,2020 na kama aliwapokea washtakiwa na kuwajaza kwenye DR.

Matata: Shahidi hakuishia hapo alitaja namba 16/2021 ambapo upande wa mashtaka haukupinga wala katika hawakusema katika Mahakama hii kuna kesi nyingine tofauti na hii.

Matata: Shahidi aliweza kueleza kuwa yeye ndie aliyetoa maelekezo kwa Wakili Fredrick na Kiongozi wa jopo la utetezi kuandika barua kwenda kwa RPC Ilala ili kuweza kupata taarifa zinazohusiana na shahidi wa pili katika kesi ndogo askari msemwa ili kupata nyaraka ili kujiridhisha.