Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mawaziri wa Madini Tanzania, Burundi wakutana

Waziri wa nishati na madini nchini Burundi,  Uwizeye Ibrahim kushoto akisalimiana na viongozi wa serikali wilayani Ngara pamoja na Waziri wa madini hapa nchini Dotto Biteko alipopokelewa mpakani mwa nchi hizo kata ya Kabanga

Muktasari:

  • Mawaziri wa wizara ya madini Tanzania na Burundi wamekutana wilayani Ngara kwa lengo la kuweka mipango ya pamoja juu ya uchimbaji wa madini ya Nickel ambayo yapo njia moja katika nchi hizo mbili.

  

Ngara. Mawaziri wa wizara ya madini Tanzania na Burundi wamekutana wilayani Ngara kwa lengo la kuweka mipango ya pamoja juu ya uchimbaji wa madini ya Nickel ambayo yapo njia moja katika nchi hizo mbili.

Uchimbaji wa madini hayo kwa upande wa Tanzania uko hatua za awali ikiwamo kuthaminisha mali za wananchi kwa ajili ya kutoa fidia na uchimbaji huo utaanza rasmi 2025.

Waziri wa Madini Tanzania, Dotto Biteko na Waziri wa Nishati na Madini nchi ya Burundi, Uwizeye Ibrahimu wakiongea leo katika mkutano uliofanyika wilaya ya Ngara mkoani Kagera, kwa pamoja wamesema baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassan kutembelelea nchini Burundi na kuongea na Rais wa nchi hiyo Evarist Ndaishimiye walihaidiana kuwa na ushirikiano wa kidiplomasi na kiuchumi katika miradi ya maendeleo.

Waziri Biteko amesema lengo la waziri huyo wa madini nchini Burundi kuja nchini ni kujifunza na kuangalia namna madini ya Nickel yanavyoweza kusaidia nchi hizo mbili kwa kuwa yako ukanda mmoja  kwa Tanzania Kabanga na Burundi Msongati

Naye Waziri wa nishati na madini nchini Burundi, Uwizeye Ibrahim amesema Kabanga kuna nickel na Burundi ipo pia hivyo ameona lazima aje Tanzania ajifunze na aone kama wataweza kufanya kazi kwa pamoja.