Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbabe Isangula afariki dunia

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Willy Isangula alikuwa miongoni mwa nyota walioweka rekodi ya kuiletea nchi medali nyingi kwenye michezo ya Afrika ya mwaka 1987 nchini Kenya akiwa na timu ya Taifa ya ngumi.

Dar es Salaam. Bondia mkongwe, Willy Isangula amefariki dunia leo asubuhi, baada ya kuugua kwa zaidi ya miaka minane. Msiba wa bondia huyo aliyewahi kuiletea nchi medali ya Afrika mwaka 1987 uko Kigamboni Kisiwani, Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi Digital, mtoto wa marehemu, Joseph Isangula amesema baba yake aliugua kwa zaidi ya miaka minane.

“Alipooza kwa muda mrefu, ikasababisha akawa hatembei kabisa, aliendelea na matibabu lakini hivi karibuni alizidiwa tukampeleka hospitali hadi leo asubuhi alipofariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili,” amesema kijana huyo.

Amesema taratibu za mazishi bado zinapangwa na familia, baada ya kikao ndipo watajua ni lini na wapi baba yao atazikwa.

Isangula aliyekuwa na umbo pana na mrefu kwa kimo, alikuwa miongoni mwa nyota walioweka rekodi ya kuiletea nchi medali nyingi kwenye michezo ya Afrika ya mwaka 1987 nchini Kenya, akiwa na timu ya Taifa ya ngumi.

Katika michezo hiyo iliyofanyika Kenya, Tanzania ilimaliza nafasi ya 12 kwenye matokeo ya jumla na kuweka rekodi ya kutwaa medali saba kwenye riadha na ngumi, rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa hadi sasa.

Miongoni mwa medali hizo ilikuwa ya Willy Isangula, bondia wa uzani wa juu, huku mabondia wengine waliotwaa medali wakiwa ni Benjamin Mwangata (fedha), Nassor Michael na Rajabu Hussein wakishinda shaba.

Medali nyingine zilikuwa za riadha za Zakayo Malekwa (fedha – kurusha mkuki), Nata Nangae (shaba – mbio za mita 3,000) Matilda Kisava (sasa marehemu) alishinda medali ya shaba ya kurusha mkuki.