Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bondia aliyedondoka ulingoni Dodoma afariki dunia

Marehemu, Najim Mohammed (kulia) akipambana mpinzani wake Laurent Segu katika pambano la raundi nne lililochezwa Aprili 23, 2023 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Najum alianguka ulingoni alipomaliza pambano lake la raundi nne jijini Dodoma dhidi ya bondia Laurent Segu ndipo akapelekwa hospitali hadi kukutwa na umauti.

Dodoma. Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Najim aliyedondoka ulingoni baada ya pambano la raundi nne na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu amefariki dunia.

 Najum alianguka ulingoni Jumapili Aprili 23, mwaka huu baada ya kumalizika kwa pambano lake la raundi nne dhidi ya bondia Laurent Segu wa Dodoma.

Katika pambano hilo, Najim alipoteza kwa pointi dhidi ya  mpinzani wake inadaiwa alifanyiwa upasuaji mdogo wa kichwa hadi asubuhi ya jana hali yake ilizidi kuimarika kabla ya kufikwa na mauti mchana huo huo.

Mwili wa bondia huyo unasafirishwa leo kutoka Dodoma kwa ajili ya maziko yanayotarajiwa kufanyika wilayani Kyela Mkoani Mbeya.

Kaka wa marehemu, Richard Chawinga amesema wapo njiani kwenda Kyela kwa ajili ya mazishi ya mdogo wake huku akisema bado hawajapanga siku ya maziko.

“Tupo njiani tukielekea Mbeya tukifika ndio tutajua utaratibu wa mazishi upoje maana kuna ndugu zetu wanatusubiria kule, ila tutamhifadhi nyumbani Kyela.” amesema Chawinga.

Bondia huyo alikuwa amecheza mapambano matatu ya ngumi za kulipwa pamoja na la Jumapili iliyopita, ambapo ameshinda moja na kupoteza mawili.


Mwisho