Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbozi kutumia viongozi wa kimila kukabili uharibifu mazingira

Mbozi. Kutokana na uharibifu wa mazingira unaoikabili Wilaya ya Mbozi  jitihata mbalimbali zimeanza kuchukuliwa na wilaya hiyo kukabiliana na changamoto hiyo.

Katika utatuzi wa changamoto hiyo ambayo inasababisha mabadiliko tabia nchi, halmashauri hiyo imeamua kushirikisha jukwaa la viongozi wa kimila kujadili changamoto na mikakati ya kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji na maandalizi ya kampeni ya upandaji miti katika wilaya hiyo.

Kikao hicho kilifanyika jana Jumatano 23,2022 ambapo kilishirikisha wadau mbalimbali ikiwamo viongozi machifu 24 wa wilaya hiyo pamoja na makatibu wao huku  Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Cosmas Nsenye akiwa mgeni rasmi.

Nsenye ametahadharisha wanaoharibu mazingira akisema watachukuliwa hatua.

 ‘’Inashangaza kwa kipindi hiki watu wanafikia hatua ya kumiliki milima, mabonde, mito kitu ambacho sio sawa, unaweza ukawa na ekari hata elfu moja lakini ndani yake kukiwa na mlima au mto sio wako’’amesema Nsenye.

 Ameongeza  "Watu hata bila kuwa na uoga wanafikia hatua ya kufunga mto na kama tunavyojua kila kiumbe hai kinahitaji maji mtu mmoja au kikundi cha watu wachache wanapofikia azimio la kufunga mto ili wanufaike wao hili jambo sio sawa.
Vilevile ameongeza kuwa kama jamii ya watu wa Mbozi itaamua kulivalia njuga suala la utunzaji wa mazingira kwa maeneo mbalimbali suala la uoto wa sasili uliokuwepo awali utarudi.

Amesisitiza kila mmoja kutekeleza kampeni ya upandaji miti ili kuweka mazingira salama

"Kwa kipindi hiki ni lazima tutilie mkazo hoja ya upandaji miti kwa kila kaya za mijini miti mitano na zile za vijijini miti 10, tasisi zote zipande miti kulingana na ukubwa wa maeneo yao na vilevile kila kitongoji kiwe na siku maalumu ya upandaji miti  maagizo yalio tolewa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri W. Kindamba katika kikao mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wake Mkuurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde amesema kuwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira ndio maana tunaona kuna baadhi ya maeneo baada ya mvua kunyesha nyumba zimeanza kuezuliwa lakini kungekuwa na miti ingezuia kasi ya upepo mkali.

‘’Nawaomba viongozi wangu wa mila kwenda kutilia mkazo wa suala la upandaji miti na kusimamia maeneo ya vyanzo vya maji kutunzwa, misitu kutokatwa kiholela kama ilivyo sasa’’ amesema Nandonde.

Ameongeza kuwa "Kunauharibifu mkubwa sana wa mazingira ambao unasababisha maeneo mbalimbali kuwa kama jangwa ndio maana hata upepo mkali ukija unaharibu makazi yetu inabidi tuchukue tahadhali kwa kupanda miti katika maeneo yetu"
.
Kwa upande wake Ofisa maliasili na mazingira wa halmashauri ya Mbozi, Hamisi Nzunda amezitaja changamoto ya uharibifu wa mazingira kuwa ni pamoja na ukataji miti ya asili kwaajili ya nishati ya kuni na mkaa na kuchomea tofali na chokaa, uvamizi wa misitu na vyanzo vya maji kwaajili ya kilimo, mifugo na makazi, uchomaji misitu kiholela, jamii kutoshiriki kupanda miti, uuzaji mashamba kiholela, vilevile viongozi kutosimamia sharia za mazingira.
Kwa upandewake kiongozi wa mila chifu Galifunga Nzowa chifu wa igamba amesema huko nyuma walijhua serikali pekee ndo inahusika na utunzaji wa mazingira lakini kwa maelekezo haya sasa  kwetu machifu suala hili ni kazi lraisi tutalivalia njuga.

Hata hivyo kwa upande wake bandelebu Tabuka msaidizi wa chifu ihanda amesema kuwa uharibifu wa mazingira mkubwa unasababishwa na wenbyeviti wa vitongoji na watendaji wa vijiji kwakuwa mmetupa tukasimamia tunaenda kutimiza wajibu wetu.

Kwa upandea wake Paula Magesa ambaye ni mdau wa mazingira anayesimamia bonde la mto mlowo amesemakuwa tubadilishe tabia za watu watu inabidi wapenbde mazingira