Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge ahoji baa na kumbi za starehe kufungwa

Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma akiomba mwongozo wa Spika kuhusu Serikali kufungia baa kwasababu ya kelele

Muktasari:

  • Sakata la kufungwa kwa baa katika maeneo mbalimbali limetua bungeni ambapo mbunge amehoji utaratibu huo unawafanya wanashindwa kupata sehemu za kutuliza mawazo.

Dodoma. Sakata la kufungwa kwa baa katika maeneo mbalimbali limetua bungeni ambapo mbunge amehoji utaratibu huo unawafanya wanashindwa kupata sehemu za kutuliza mawazo.

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) leo Mei 15, 2023 ameomba mwongozo wa Spika akitaka kujua ni kwa nini Serikali inafungia baa nzuri ambazo wabunge walizoea kwenda kutuliza mawazo yao baada ya kazi ngumu.

“Mheshimiwa Spika, Mbunge Jesca (Msambatavangu) alishasema hapa kuhusu afya ya akili na namna ya kutakiwa kutuliza mawazo, leo hii tunavyoongea maeneo mengi nchi baada nzuri na sehemu za starehe zimefungwa, wabunge na watu wengine wanakosa maeneo ya kustarehe, naomba mwongozo wako,” amehoji Msukuma.

Hivi karibuni Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ilitangaza kuzifungia baa na kumbi za starehe katika majiji ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Arusha kwa kilichoelewa kuwa walikiuka sheria ya mazingira kwa kupiga miziki kwa sauti za juu.

Mbunge huyo mbali na kuhoji kuhusu starehe, lakini amesema kuwa wamiliki wa baa hizo wanapata adha kubwa ikiwemo Serikali kukosa mapato yake kwa jambo alilosema si sahihi.

Akijibu mwongozo huo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema kanuni aliyotumia Msukuma namba 76 inasema atatolea mwongozo kwa jambo lililotokea mapema siku hiyo lakini kwa hilo la jambo halikuwa limetokea mapema hivyo akamwomba kutumia njia nyingine kuwasilisha kero yake.