NEMC yazifungulia baa, kumbi za starehe 20

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk Samuel Gwamaka.

Muktasari:

  • Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limezifungulia baa na kumbi za starehe 20 kati ya 89 zilizofungiwa katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma kutokana na kukiuka kanuni na sheria za uhifadhi wa mazingira.

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk Samuel Gwamaka amesema baada ya kutafakari athari za kiuchumi, wafanyabiashara 20 walioandika barua na kukiri makosa yao wamefunguliwa.

 Mei 8, 2023, (NEMC) ilizifungia baa na kumbi za starehe 89 za majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma baada ya kubaini kupiga kelele na mitetemo iliyozidi viwango vinavyotakiwa.

Akizunguza kwenye mjadala wa Mwananchi Twitter Space leo Jumatano Mei 10,2023  yenye mada ya kufungia baa, kumbi za starehe kwa sababu ya kelele ni suluhisho ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL)

Dk wamaka amesema, wapo waliokiri na kuandika barua, na kulipa faini.

“Ni mara ya kwanza tulilazimika kuwafungia baada ya kutoa elimu kwa miaka mitano, watu walikuwa hawalali licha ya malalamiko yakiongezeka,” amesema Gwamaka.

Amesema walitumia mbinu mbalimbali ikiwemo kuwaita wamiliki wote na kutoa elimu kuanzia ngazi ya mkoa na baadae ngazi ya ya halmashauri.

“Kelele ziliendelea na malalniko yaliendele tukatoa angalizo watakaoendelea kukiu sheria kuanzia Mei Mosi, hatua zitachukuliwa, baada ya kuona tumeanza kuchukua ndio wakashtuka,” amesema na kuongeza:

“Kila mtu ananafasi yake kuna washehereshaji lakini pia kuna wenye ajira, lakini kuna watu walioathitirika na wengine kufariki,” amesema.

Miongoni mwa baa na kumbi za starehe zilizofungiwa ni Bodroom, Wavuvi Camp, Wherehouse, Avoco, Kitambaa Cheupe.Wengine ni Element, Chako ni Chako, Rainbow, Gentlemen, Liquid na Soweto.