Mbunge ashauri reli ya kisasa kujengwa na mkandarasi mmoja

Wednesday June 22 2022
relipic
By Sharon Sauwa

Dodoma. Mbunge wa Mtwara Mjini, Hassan Mtenga ameishauri Serikali kuachana na  makandarasi zaidi ya mmoja katika ujenzi wa reli ya kisasa  SGR kutokana na umuhimu wa reli hiyo kwa usalama wa Taifa.

Mtenga ameyasema hayo leo Jumatano Juni 22,2023 wakati akichangia mjadala wa bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2022/2023.

Amesema katika ujenzi wa reli ya Tazara walijenga raia wa  China na reli ya kati  walijenga Wajerumani hadi  mwisho hakukuwa na ubadilishaji wa mkandarasi.

“Naiomba Serikali kwenye dhana ya usalama wa nchi, hebu turudi sasa tuangalie ni mkandarasi gani bora ambaye anaweza kuingia joint venture na kampuni nyingine wakajenga reli hii,” amesema.

Advertisement