Mbunge CCM ‘aichongea’ halmashauri, Magufuli aagiza uchunguzi mkopo wa Sh12 bilioni

Mbunge CCM ‘aichongea’ halmashauri, Magufuli aagiza uchunguzi mkopo wa Sh19 bilioni

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, John Magufuli ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mkopo wa Sh12 bilioni uliotolewa na benki ya CRDB kwa halmashauri ya Temeke.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mkopo wa Sh12 bilioni uliotolewa na benki ya CRDB kwa halmashauri ya Temeke.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa agizo hilo leo Ijumaa Februari 26, 2021 katika ziara yake jijini Dar es Salaam baada ya mbunge wa Temeke (CCM), Dorothy Kilave kuomba Serikali iwasaidie kulipa mkopo huo unaowagharimu Sh4.8 bilioni kila mwaka.

“Yaani Serikali ikalipe mkopo ambao haikuhusika, haya ni mambo ya ajabu. Mlienda kuzungumza wenyewe na benki mmeshindwa kulipa mnataka Serikali ilipe. Kuna manispaa ngapi kwa hiyo ziwe zinafanya mikopo ya wizi halafu serikali ilipe. Hilo mtalibeba wenyewe, kwanza ni kukosa nidhamu.”

“Hakuna hela itakayotolewa na serikali labda kutuma wachunguzi kuchunguza kujua hizo fedha zinarushwa kiasi gani, namuelekeza kamanda wa Takukuru kuchunguza hawa naona kuna ufisadi mkubwa unaelea,” amesema Magufuli.

Amesema hiyo ilikuwa kawaida ya halmashauri kujiingiza kwenye ufisadi na kutumia vibaya fedha za miradi.