Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbwana ataja siri iliyojificha mgomo Kariakoo

Mwenykiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Soko Kuunla Kariakoo, Martin Mbwana akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Mei 16, 2023 Kariakoo, Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Kiongozi wa wafanyabiashara Kariakoo amesema yupo tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili viweze kuwachukulia hatua watu ambao bado hawajafungua maduka.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana amesema mgomo unaoendelea leo unasababishwa na kikundi cha watu wachache wenye maslahi yao binafsi.

Kutokana na hilo amesema kama kiongozi yuko tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili viweze kuwachukulia hatua watu hao.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 15, 2023 wakati akizungumza na Mwananchi kufuatia baadhi ya maduka kuendelea kufungwa, licha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana kuwataka wafanyabiashara hao kusitisha mgomo huku akiahidi kushughulikia kero zao kikao cha kesho Jumatano ya Mei 17, 2023.

Kauli ya Mwenyekiti huyo inakuja ikiwa baadhi ya maduka katika soko hilo bado kufungwa kwa siku ya pili sasa.

Katika uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umegundua mengi ya maduka yaliyofungwa, ni yale yanayouza nguo, viatu, vyombo, vitenge, mapazia huku yaliyofunguliwa yakiwa ni yale ya vifaa vya magari, urembo wa ndani, na maduka ya vitambaa vya kushona.

Hata hivyo maduka mengi yaliyowazi, ni yale yaliyopo pembezoni mwa soko huku asilimia kubwa ya maduka ya katikati yakiwa yamefungwa.

Mbwana amesema kilio chao kama wafanyabiashara ilikuwa ni kusikilizwa na Rais Samia Suluhu Hassan, na katika kuonyesha kuwa amewasikia alimtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

"Alipokuja aliwaomba wafanyabiashara wafungue maduka na kuahidi kuwasiliza siku ya Jumatano. Nashangaa wafanyabiashara kuwa hawana imani na Waziru Mkuu," amesema

Amesema shida ni kikundi cha watu wachache wanaoonekana kuwa na manufaa na mgomo huo huku akieleza kuwa ameomba msaada kwa vyombo vya usalama.

“Kuna kikundi cha watu wachache wanafaidika na huu mgomo ikiwemo kuonyesha kuwa kazi hazifanywi na Rais Samia Suluhu Hassan. Unafunga duka Rais ameshamtuna Waziri Mkuu, ametaka mfungue maduka bado hutaki; unataka nini!" Amehoji mwenyekiti huyo.

Miongoni mwa kero zilizokuwa zikilalamikiwa na wafanyabiashara hao, ni kamatakakamata ya wafanyabiashara, utoaji wa risiti xa kielektroniki na kudai kuwa unaua biashara. Wafanyabiashara hao pia wanalalamikia sheria mpya ya usajili wa stoo.

Mgomo huo ambao kwa mujibu wa viongozi wake, un lengo la kuishawishi serikali kusikiliza kilio chao, na hivyo serikali kuonyesha nia ya kukaa meza moja na wafanyabiashara hao, hali imekuwa tete kwa wafanyabiashara wanaonunua bidhaa sokoni hapo wakitoka nje ya Dar es Salaam.

Antony Msandali ambaye ni mfanyabiashara kutoka Kigoma amesema kuwapo kwa mgomo huo kumemuongezea gharama kwani alikuwa amepanga kuondoka jana lakini hakupata bidhaa.

"Mipango yangu ilikuwa niondoke jana lakini sikuweza, sikupata mzigo, nikajua jana Waziri mkuu amemaliza mgogoro leo tena nimeamka nakuta bado kumefungwa, sielewi. Hapa nilipo nimeanza kula mtaji kwa sababu kila ninachokifanya sasa kipo nje ya bajeti, chakula, malazi na lojistiki (logistics)," alisema Msandali.