Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchechu ataka tija taasisi za umma

Muktasari:

  • Mchechu azitaka taasisi za Serikali kukaa mguu sawa akisisitiza lengo la Serikali ni kuona taasisi hizo zinakua na zinaleta tija.

Dar es Salaam. Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu amewataka wenyeviti na maofisa watendaji wa taasisi za Serikali kuhakikisha taasisi hizo zinakuwa na matokeo chanya kwa uchumi.

Mchechu ameyasema hayo wakati maadhimisho ya miaka 25 ya benki ya NMB yaliyoenda sambamba na utoaji wa gawio kwa Serikali kiasi cha Sh45.5 bilioni.

Akizungumza katika hafla hiyo Mchechu amemtaja Rais Samia Suluhu Hassan kama kinara wa mageuzi ya kidemokrasia na uchumi hivyo taasisi za Serikali pia zinapaswa kuwa na mtazamo huo.

“Siku zote mabadiliko ya uchumi yanakuwa na mtazamo tofauti na vikwazo vingi. NMB ni hadithi nzuri tunaishi leo ikituonyesha tulipotoka. Wakati NMB inaenda kwenye awamu ya pili ya ubinafsishaji wengi walipinga ikiwemo bodi na ilibidi Rais amtoe mwenyekiti na bodi ivunjwe ili mchakato uendelee.

“Hadi dakika tuna benki ambazo zinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100, ukienda kwenye bajeti iliyosomwa juzi tumeweka lengo la kuzipa mtaji hizo benki na mimi katika ofisi ya msajili wa hazina sijapokea hata senti ya rejesho. Sasa tujiulize jema ni lipi tumiliki asilimia 100 halafu tuendelee kutoa kwenye chungu kuwapa hao au tukaenda katika mfumo huu wa NMB,”

Amesema lengo la Serikali ni kuziona taasisi zake zinakua hivyo aliwataka wenyeviti wa bosi na maofisa watendaji wakuu kukaa tayari kufanikisha lengo hilo.

“Haya tunayoyaona kwa NMB tunataka kuyaona kwenye taasisi zote hivyo wenyeviti na watendaji wakuu wajiandae vizuri.Ndiyo maana tunaposema unapofanya mageuzi na wewe umekuwa rais wa mageuzi ya kiuchumi na kidemokrasi wapo wanaokuelewa na wasiokuelewa sasa watakuelewa baadaye,”amesema Mchechu.

S: Mchechu azitaka taasisi za Serikali kukaa mguu sawa akisisitiza lengo la Serikali ni kuona taasisi hizo zinakua na zinaleta tija

Elizabeth Edward, Mwananchi