Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchengerwa amsimamisha kazi mkurugenzi Busega

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busega mkoani Simiyu, Veronica Sayore.

Muktasari:

  • Ikiwa zimepita saa kadhaa tangu kusimamishwa kazi, watumishi wawili Wilaya ya Uvinza, mkoani Kigoma naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busega mkoani Simiyu, Veronica Sayore amesimamishwa kazi kwa kile kinachodaiwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busega mkoani Simiyu, Veronica Sayore, kuanzia leo.

 Huo ni muendelezo wa Waziri huyo kuendelea kuwawajibisha watendaji wa Serikali wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao, ikimbukwe Septemba 18, mwaka huu aliwasimamisha watumishi wengine saba wa Halmashauri ya Liwale mkoani Lindi kwa changamoto hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Nteghenjwa Hosseah imeweka bayana kuwa Ofisa huyo anasimamishwa kupisha uchunguzi kufuatia malalamiko yanayomkabili.

“Veronica Vicent Sayore amesimamishwa kuanzia leo Septemba 22, 2023 ili kupisha uchunguzi. Waziri mechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kuhusu utendaji kazi usioridhisha, kutokuwa na ushirikiano na viongozi wenzake pamoja na kutowashirikisha watendaji katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,” amesema.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo imeadai kuwa Waziri Mchengerwa amemwelekeza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Tamisemi kuunda timu ya uchunguzi wa mwenendo wa utendaji kazi wa mkurugenzi huyo pamoja na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega.

Amesema Waziri huyo amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kusimamia dhana ya ushirikishwaji wa viongozi, watendaji na wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuimarisha mahusiano mazuri baina ya viongozi na watendaji ili kujenga timu yenye umoja katika kutekeleza jukumu la kuwahudumia wananchi.