Mdalasini na asali zinavyoweza kuongeza nguvu za kiume

Muktasari:
Moja ya njia hizo ni matumizi ya asali ya asili ya mdalasini.
Asali ambayo imefanyiwa tafiti mbalimbali za kitatibu imeonyesha uwezo wake wa kutibu magonjwa mbalimbali, kwenye hili pia imethibitisha hilo pale inapochanganywa na mdalasini.
Dar es Salaam. Wataalamu wengi wa afya na hata majarida ya afya yameandika kuhusu njia mbalimbali za kuongeza nguvu za kiume.
Moja ya njia hizo ni matumizi ya asali ya asili ya mdalasini.
Asali ambayo imefanyiwa tafiti mbalimbali za kitatibu imeonyesha uwezo wake wa kutibu magonjwa mbalimbali, kwenye hili pia imethibitisha hilo pale inapochanganywa na mdalasini.
Ili kupata mchanganyiko huo, chukua lita moja ya asali asili safi kisha changanya na mdalasini uliosagwa kama unga vijiko vinne vya chakula.
Baada ya hapo utakuwa unakunywa kijiko kimoja cha chakula kabla ya kulala kila siku kwa mwezi mmoja.