Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mdee ahoji ubora mkandarasi bwawa la Mwalimu Nyerere

Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee akizungumza bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2022/2023, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee amemtaka Waziri wa Nishati, January Makamba atoe maelezo ya kina kuhusu mkandarasi wa ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere kwamba amekuwa mbabaishaji.

  

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee amemtaka Waziri wa Nishati, January Makamba atoe maelezo ya kina kuhusu mkandarasi wa ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere kwamba amekuwa mbabaishaji.

Mdee amesema hakuna mkandarasi anayelipwa vizuri hapa nchini kama mjenzi wa bwawa hilo lakini anaona serikali inamlinda.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo Juni 2, wakati akichangia hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2022/23.

Amesema mkandarasi huyo na Wizara wanatoa taarifa ambazo zinakinzana lakini sababu zao hazina mashiko.

"Mkataba unasema mkandarasi angemaliza kazi Juni 14,2022 leo hii kazi ipo asilimia 67, nataka kujua Taifa linapata nini kutoka kwa mtu huyu ambaye amekiuka mkataba, au ndiyo wanasheria wetu kutuingiza chaka.

"Watanzania tunapigwa nataka kujua mpunga wetu unaliwaje katika mkataba huu wa Sh6.5 trilioni na pesa inakwenda kama kawaida yani akitikisika tu mpunga huo," amehoji Mdee.

Mbunge huyo wa zamani wa Kawe amesema hana ugomvi na mtu lakini anatambua kuwa na yeye ni Mtanzania anayepaswa kujua rasilimali za nchi Kwa jinsi zinavyotumika na kwa nini mtu akiuke mkataba halafu asichukuliwe hatua.

Mdee amesema taarifa ya Wizara ambayo ilitolewa February na Naibu Waziri wa Nishati ilieleza Serikali kuzikataa sababu za mkandarasi huyo lakini inashangaza taarifa ya April imeikubali kuwa tatizo la Uviko 19 ndiyo chanzo cha kuchelewesha kazi akisema ni uongo.

Kwa mujibu wa Mdee, Mkandarasi alidanganya, kwani alijenga tuta moja badala ya mawili na mafuriko yalipokuja yakasomba tuta lote kikawa chanzo cha uanza upya kazi hiyo.