Mganga wa kienyeji afungwa miaka mitatu jela

Mganga wa jadi jela kwa kosa la kumuua mwenzake wakigombea mwanamke

Muktasari:

  • Mganga huyo wa kienyeji Salim Amiri mkazi wa Kijiji cha Kangala, Kata ya Loiborsiret wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh200,000 kwa kosa la kufanya tiba za jadi bila kuwa na kibali.

Simanjiro. Mganga wa kienyeji mkazi wa Kijiji cha Kangala Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Salim Amiri (34) amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu kwa kosa la kufanya shughuli za tiba za asili bila kuwa na kibali.

 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Charles Uiso ametoa hukumu hiyo baada ya mshakiwa kukiri kosa hilo na kukutwa akiwa na zana za kazi yake.

Hakimu Uiso amesema mshtakiwa huyo ambaye amekiri kosa hilo alikutwa na shanga, vibuyu na pembe akitoa tiba za jadi kwa watu bila kuwa na kibali kwenye Kijiji cha Kangala.

Hakimu huyo alitoa hukumu ya Amiri kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwenda jela au kutozwa faini ya Sh200,000.

Awali, mwendesha mashtaka wa serikali Mosses Hamilton ameieleza mahakama kuwa Amiri hana taarifa za kufanya uhalifu na kutumikia kifungo hivyo itoe adhabu kulingana na sheria.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo aliiomba mahakama hiyo imuonee huruma na kumpunguzia adhabu kwani ni kosa lake la kwanza na ana familia ya mke na watoto wanamtegemea.

Hata hivyo, mshtakiwa wa pili wa kesi hiyo ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kangala, Mohamed Kadangu (37) alikana shataka hilo alipoulizwa mahakamani hapo kama ni kweli alitenda kosa hilo.

Kesi hiyo itaendelea tena Mei 10 mwaka huu kwa mshtakiwa wa pili Kadangu ambaye yeye hakukubali kosa hivyo hakimu ameahirisha hadi itakapoendelea mahakamani hapo.