Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Misaada zaidi yahitajika katika vituo vya kulelea watoto yatima

Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la CAREUSTZ, Ikunda Mtenga (kulia) akikabidhi fedha kwa watoto wanaishi katika kituo Cha kulea watoto yatima cha Watoto Wetu Tanzania( WWT) kilichopo Mbezi, barabara ya Kwenda Goba, hata hivyo shirika hilo limetoa misaada mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule, bima za afya kwa wanafunzi na fedha za kujikimu vyenye thamani ya zaidi ya Sh 2milioni kwa kituo hicho.

Muktasari:

Pamoja na jamii kuwapelekea misaada mbalimbali watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu, Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la CAREUSTZ, Ikunda Mtenga amesema bado misaada zaidi inahitajika katika vituo vya kulelea watoto yatima.

Dar es Salaam. Pamoja na jamii kuwapelekea misaada mbalimbali watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu, Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la CAREUSTZ, Ikunda Mtenga amesema bado misaada zaidi inahitajika katika vituo vya kulelea watoto yatima.

Mtenga amesema hayo leo Mei 4, 2022 wakati akikabidhi misaada mbalimbali kwenye kituo cha watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi cha Watoto Wetu Tanzania (WWT) kilichopo Mbezi- Goba.

Amesema kila mmoja anawajibu wa kuwajali watu wenye mahitaji maalumu, kuwatunza watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu ili nao wajione kuwa hawajatengwa na jamii.

" Leo tumejumuika katika kituo cha Watoto wetu( WWT) kwa ajili kutoa zawadi chache kwa ajili ya Watoto, tumewakabidhi bima za afya kwa ajili ya Watoto 10, vifaa ya shule, mavazi, fedha kwa ajili ya kujikimu kituo hicho pamoja na  kula chakula cha mchana na watoto hawa, kama ishara ya upendo" amesema Mtenga.

Mtenga amesema lengo la kuanzishwa kwa shirika hilo ni kusaidia watu na watoto wenye uhitaji maalumu na tayari misaada kama hiyo wanaitoa kwa wakimbizi waliopo nchini Marekani.

"Sisi CAREUSTZ hatusaidi mtu mmoja mmoja, bali tunaenda katika taasisi kama hii ambayo imekusanya watu na inawasaidia na sisi tunatoa msaada wetu pale au katika hospitali ambayo imekusanya wagonjwa wengi na imezidia, sisi ndio tunaenda kusaidia hapo" amesema Mtenga.

Amebainisha kuwa watoto yatima wanahitaji huduma bora za afya kama walivyo watoto wengine ili ukuaji wao usiwe na matatizo.

"Upendo ni kitu kikubwa na hata vitabu vya dini vinatusisita kuwa tupendane, hivyo kila mmoja anawajibu wa kuwapenda na kuwajali watu wenye mahitaji maalumu" amesema

Advela Felix ni Mratibu wa Kituo hicho, anasema watoto yatima 69, waliopo kwenye kituo hicho wanahitaji misaada mbalimbali hasa ikiwemo chakula na mavazi.

"Tunawaomba watanzania wenzetu kujitolea kwa kila kitu walichojaliwa kuwa nacho, kwani ili mtoto aweze kufanya vizuri katika masomo yake , lazima aweze kupatiwa mahitaji muhimu" amesema Felix.

Akiongea kwa niaba ya watoto wa kituo hicho, Restuta Richard, amesema misaada hiyo itawasaidia kufikia malengo yao na hivyo kuomba mashirika na Taasisi nyingine ziendelee kusaidia vituo vyenye changamoto.

Mkurugenzi wa Fedha wa shirika la CAREUSTZ, Peter Kiango, amesema misaada iliyotolewa na shirika.lake Ina thamani ya ziaidi ya Sh 2milioni na kwamba wamejipanga kusaiida vituo vingine hapa nchini.