Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mjue Othman Massoud, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Othman Masoud atangazwa kuwa mrithi wa Maalim Seif

Muktasari:

  • Othman Massoud Othman, ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu za Zanzibar, alizaliwa katika kijiji cha Pandani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, mwanzoni mwa miaka ya sitini, baba yake akiwa ni Sheikh Massoud Bin Othman.

Othman Massoud Othman, ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu za Zanzibar, alizaliwa katika kijiji cha Pandani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, mwanzoni mwa miaka ya sitini, baba yake akiwa ni Sheikh Massoud Bin Othman.

Alipata elimu ya msingi katika shule ya Pandani na baadaye Sekondari ya Fidel Castro, Chake Chake, Kusini Pemba.

Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa Shahada ya Kwanza katika Sheria (LL.B). Baada ya Chuo Kikuu alirejea Zanzibar na kuajiriwa na SMZ katika Wizara ya Katiba na Sheria kama Wakili. Kisha akaenda kusoma Chuo Kikuu cha London ambako alipata Shahada ya Pili ya Sheria (LL.M).

Baada ya masomo aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Utawala Bora na Sheria chini ya Dk Salmin Amour, baadaye akawa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar chini ya Amani Karume na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali chini ya Dk Mohamed Shein.

Wakati wa Bunge la Katiba, msimamo wake ulimfanya afukuzwe katika CCM, kisha kupoteza wadhifa wake wa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Agosti 2014 alijiunga na CUF hadi mwaka 2020 alipohamia ACT-Wazalendo. Hatimaye leo ametangazwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.