Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkoa wa Shinyanga umejipanga kupanda miti milioni tisa

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akipanda mti wakati wa kampeni ya upandaji miti uliofanyika eneo la Butengwa Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Picha na Suzy Butondo.

Muktasari:

Mkoa wa Shinyanga unatekeleza kampeni ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupanda zaidi ya miti milioni tisa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Shinyanga. Mkoa wa Shinyanga unatekeleza kampeni ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupanda zaidi ya miti milioni tisa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Katika utekelezaji wa kampeni hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme ameagiza kila halmashauri mkoani humo kupata miti isiyopungua milioni 1.5 kila mwaka.

Akizungumza mjini Shinyanga leo Aprili 25, 2023n wakati wa hafla ya kupata miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mndeme ameataka wakazi wa mkoa huo kujenga utamaduni wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa kuacha kukata kuni kwa ajili ya kuchoma mkaa.

Amewata wote walioshiriki kazi ya kupanda miti katika tukio hilo lililoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika shule ya wasichana Butengwa kuwa kampeni ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi inapaswa kuhusisha kila mtu kuanzia mijini hadi vijijini.

"Nawaombeni wakazi wote wa Mkoa wa Shinyanga kupanda miti kila mtu katika eneo lake; maofisa misitu wabebe dhamana ya kuhamasiasha umma kupanda miti kwa kuotesha na kugawa miche bure kwa wananchi. Kwa kuanzia, tuhakikishe kila familia inapata angalau miche mitatu, miwili ya matunda na moja ya kivuli kila msimu wa mvua,” amesema Mndeme

Katika wajibu huo, kiongozi huyo ameagiza kila mfanyabiashara, kila nyumba ya ibada, ofisi za umma na binafsi kupanda miti ya matunda na kivuli katika maeneo yao.

Dotto Clementi, mkazi wa Manispaa ya Shinyanga ameshauri kampeni ya kupanda miti ihusishe watoto kuanzia nyumbani hadi shuleni ili kuwajengea utamaduni wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti.