Mkurugenzi Gairo asimamishwa kazi

Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikalia za mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu

Muktasari:

  • Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikalia za mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa halmashauri ya Gairo Asajile Mwambambale ili aende kujibu tuhuma zinazomkabili katika kituo chake cha kazi cha zamani.


Dar es Salaam. Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikalia za mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa halmashauri ya Gairo Asajile Mwambambale ili aende kujibu tuhuma zinazomkabili katika kituo chake cha kazi cha zamani.

Taarifa iliyotolewa jana Ijumaa Septemba 10, 2021 na Ofisi ya Rais Tamisemi, imesema Mwambambale kabla ya kuhamishiwa Gairo alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa anahusishwa na tuhuma za upotevu wa mabati 1,172 ambayo yalipotea katika halmashauri hiyo aliyokuwa akiiongoza.

Mkurugenzi Gairo asimamishwa kazi

“Waziri amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo ili kwenda kujibu tuhuma zinazomkabili katika halmashauri ya Kilosa na pia amemuagiza Katibu Mkuu Tamisemi kupeleka tume huru ya kuchunguza kwa kina suala la aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,” imeeleza taarifa ya Tamisemi.


Taarifa hiyo ilielezwa kuwa Wizara ilipokea taarifa ya maandishi kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Morogoroa Septemba 9 kuhusu suala hilo na Katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro alishamwelekeza Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilosa kuwachukulia hatua watumishi wengine waliohusika na suala hilo.