Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlinzi auwawa kwa kuchomwa kisu tumboni

Muktasari:

  • Mlinzi wa kampuni ya Mast Holding Steven Felician Samandari (25) ameuwawa kwa kuchoma kisu tumboni na watu wasiojulikana wakati akiwa kwenye lindo lake la baa MD Kepla wilayani hapa.

Kahama. Mlinzi wa kampuni ya Mast Holding Steven Felician Samandari (25) ameuwawa kwa kuchoma kisu tumboni na watu wasiojulikana wakati akiwa kwenye lindo lake la baa MD Kepla wilayani hapa.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga, ACP George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hili akisema kuwa, tukio hilo lilitokea Septemba 11 saa 4 usiku mtaa wa Nyahanga.

Amesema mlizi huyo alichomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio na kuingia ndani kwenye sehemu aliyokuwa akilinda na baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitokomea kusikujulikana.

RPC Kyando amesema kuwa, chanzo cha tukio hilo ni kufuatiliwa kwa wahudumu wa baa hiyo kwa ajili ya mapenzi na kwamba katika eneo hilo la tukio kumeokotwa kisu kikiwa tumboni kwa marehemu. 

Kutokana na sababu hiyo, RPC Kyando amesema wanamshikilia mhuduma wa baa hiyo, Fatuma Charles (22) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


Mmoja wa wahudumu wa baa hiyo kulipotokea tukio hilo ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini alisema, siku hiyo walifunga baa mapema lakini kuna wateja walibaki wakiendelea kupata huduma mpaka majira ya saa 10 alfajiri, huku kukipigwa muziki kwa sauti kubwa.

Amesema walipoamka mapema kwa ajili ya kufanya usafi kwenye nyumba ya kulala wageni ndipo walipokutana na tukio hilo na kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo walifika na kumchukua mlinzi aliyekuwa ameuwawa akiwa na kisu tumboni.