Mmisri alamba Sh23 milioni mashindano ya Quran

Muktasari:
- Kijana Omar Mohammed Hussein kutoka Misri amenyakua kitita cha Sh23.9 milioni baada ya kushinda katika mashindano ya Quran.
Dar es Salaam. Kijana kutoka Misri, Omar Mohammed Hussein kutoka Misri ameibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya kuhifadhi Quran akichukua kitita cha Sh23.9 milioni.
Mashindano hayo yameshirikisha vijana 23 kutoka mataifa 22, Afrika, Asia, Ulaya na Marekani, huku , kutoka nchini Misri akiibuka mshindi wa kwanza.
Mashindano hayo yamefanyika leo, Jumapili Aprili 9, 2023 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mbali na Hussein, nafasi ya pili imeshikwa na Mouhamadou Toure kutoka Senegal aliyepata Sh15.3 milioni, wa tatu ni Mtanzania Abdulrahim Masoud aliyeshinda Sh10.28 milioni.
Ushindi wa nne umekwenda kwa Mohammed Ahmed kutoka Kenya aliyejinyakulia Sh7.16 milioni, huku nafasi ya tano akishinda Mtanzania Bakari Juma Hamad aliyeshinda Sh4.63 milioni.
Aliyeibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa washiriki kutoka nje ya Afrika ni Abuutwalib Imlan kutoka Saudi Arabia akishinda Sh9.56 milioni.
Mshindi wa pili wa kundi hilo, ametoka Uingereza, Bilal Omar akishinda Sh4.78 milioni na wa tatu ni Ahmed Al-hakshi kutoka Uingereza akishinda Sh2.39 milioni.