Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mradi wa Sh24 bilioni wanusuru ndoa kuvunjika

Muonekano wa tanki la maji ya Ziwa Victoria likiwa katika kata ya Tinde lenye ujazo wa lita 1,150,000 ambalo linahudumia vijiji vitatu

Muktasari:

Kukamilika kwa mradi huo pia kunatajwa kuokoa ndoa na mimba za utotoni kwa watoto wakike waliokuwa wakiamka saa 11:00 alfajiri kufuata maji umbali wa kilomita nne.

Shinyanga. Wananchi 20,201 wa Kata ya Tinde na Didia Wilaya na Mkoa wa Shinyanga, wamenufaika na mradi wa maji ya ziwa Victoria unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Shuwasa).

Kukamilika kwa mradi huo pia kunatajwa kuokoa ndoa na mimba za utotoni kwa watoto wakike waliokuwa wakiamka saa 11:00 alfajiri kufuata maji umbali wa kilomita nne.

Wakizungumza na waandishi wa habari Juni 30, 2023 baadhi ya wananchi wa kata hizo wameishukuru Serikali kwa kusikia kilio chao na kuwanusuru na mimba za utotoni na ndoa kuvunjika.

“Tulikuwa tukifuata maji umbali wa kilometa nne kutoka kuanzia saa 11:00 na kurudi saa 5:00 asubuhi hali ambayo ilikuwa ikisababisha wanawake kupigwa na waume zao na watoto wa kike kubakwa nyakati za usiku wakiwa wanatoka kuchota maji,” amesema Mwanne Deus mkazi wa Tinde

Mkazi mwingine Omary Salumu amesema kupatikana kwa maji familia zao zitatulia na ndoa hazitafarakana tena kwa sababu huduma hiyo kwasasa itaanza kupatikana karibu.

Mbali na kuyafuata mbali maji hayo, walikuwa wanauziwa dumu la lita 20 kwa Sh500 na wakati mwingine Sh1000.

Meneja wa Kanda ya Tinde kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira, Joshua Matinde amesema mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 100 ambao utahudumia vijiji vitatu vya Tinde kati ya vijiji 22.

Mradi huo ni muendelezo wa ujenzi wa mradi wa Tinde Sherui uliotekelezwa na Wizara ya Maji kupitia mkandarasi Megha Engineering and Infrastructure Ltd.

Meneja wa kanda ya Didia kutoka Shuwasa, Innocent Siame amesema tayari mradi wa maji ya Ziwa Victoria umekamilika katika kata ya Didia halmashauri ya Shinyanga na baada ya wiki mbili huduma zitaanza kutolewa kwa baadhi ya vijiji.

Kaimu Mkurugenzi wa Shuwasa, Sarah Emmanuel amesema mamlaka inatekeleza mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba za usambazaji takribani kilomita 8.1 kwa awamu ya kwanza utakaohudumia vijiji vya Jomu na Nyambui ambao umegharimu zaidi ya Sh24 bilioni.

Amesema kwa sehemu ya Tinde pekee mradi huo umegharimu Sh5 bilioni na utekelzaji wake ulianza Agosti 2021 ukiwa umesanifiwa kuwahudumia wananchi 60,000.