Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mrithi wa Profesa Hoseah TLS kupatikana Mei

professa Edward Hoseah anayemaliza muhula wake wa pili na wa mwisho kugombea kwa mujibu wa sheria. Picha na Maktaba

Muktasari:


  • Uchaguzi wa TLS hufanyika kila mwaka kwa mujibu wa sheria, mwaka jana, Profesa Hoseah alitetea kiti chake cha urais kwa muhula wa pili na wa mwisho kwake kugombea akiwabwaga, Harold Sungusia na Jeremia Mtobesya kwenye uchaguzi uliofanyika jijini Arusha.

Dar es Salaam. Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) umepangwa kufanyika Mei 12 ukitanguliwa na mkutano mkuu kuanzia saa moja asubuhi.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Charles Rwechungura inasema uchaguzi huo utatanguliwa na ule wa mikoa utakaofanyika kati ya Aprili 14 au 15.
Nafasi zinazogombewa kwenye mikoa ni mwenyekiti wa mawakili wa mkoa, makamu mwenyekiti, mhasibu na mwakilishi wa mawakili wa mkoa kwenye mkutano mkuu.

Wengine ni mwenyekiti wa mkoa wa kamati ya msaada wa kisheria, mwenyekiti wa mkoa wa kamati ya elimu endelevu ya sheria, mwenyekiti wa mkoa wa kamati ya ustawi ya wanachama na mwakilishi wa mkoa kwenye kamati ya utendaji (EXCOM).
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Mei 10, wanachama wa mawakili vijana, watapiga kura kumchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na katibu mkuu wa Chama cha Mawakili Vijana (AYL) wakati chaguzi za kanda zikifanyika siku moja baadaye.

Nafasi zitakazowaniwa kwenye kanda ni ya kiongozi wa kanda (council member), wawakilishi wawili wa mawakili wa kanda kwenye mkutano mkuu, mwakilishi wa kanda kwenye kamati ya utendaji (zonal EXCOM) na  mwakilishi wa kanda wa mawakili vijana kwenye kamati ya utendaji (Zonal EXCOM).

Wengine kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi iliyochapishwa kwenye gazeti l Mwananchi la leo Februari 2 ni  mwakilishi wa kanda anayewakilisha mawakili wanawake kwenye kamati ya utendaji (Zonal EXCOM) na mwakilishi wa kanda anayewakilisha wenye ulemavu kwenye kamati ya utendaji (Zonal EXCOM).

Mei 12, wanachama wa TLS watapiga kura kuchagua rais mpya atakayechukua mikoba ya professa Edward Hoseah anayemaliza muhula wake wa pili na wa mwisho kugombea kwa mujibu wa sheria inayotoa kipindi kimoja cha kiongozi aliyepo madarakani kutetea kiti chake.

Dk Hoseah aliiongoza TLS tangu 2021 na kutetea kiti chake 2022. Nafasi nyingine zitazogombewa kwenye uchaguzi huo ni ya makamu wa rais na mweka hazina, huku kamati ikitarajiwa kutangaza mchakato wa kuanza kampeni wakati wowote.

Marais wengine waliowahi kuongoza TLS kwa miaka ya karibuni ni Tundu Lissu aliyekabidhi kijiti kwa Fatma Karume mwaka 2018, kisha Dk Rugemeleza Nshala (2019-2020), na Dk Hoseah 2021 hadi sasa.