Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msama azungumzia sakata la Serikali kukopa

Muandaaji wa matamasha ya muziki wa injili nchini, Alex Msama

Muktasari:

Muandaaji wa matamasha ya muziki wa injili, Alex Msama ajitosa, kuzungumzia suala la Serikali kukopa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali, asema ni jambo la kawaida na taifa lolote linaloendelea lazima likope fedha.

Dar es Salaam. Muandaaji wa matamasha mbalimbali ya muziki wa injili nchini, Alex Msama amesema maendeleo makubwa katika mataifa hayawezi kufanikiwa pasipo nchi husika kukopa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, akisema kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Serikali kuendelea kukopa inapaswa kuungwa mkono.

Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu masuala yanayoendelea nchini hususan mjadala kuhusu kauli ya Rais Samia kuwa Tanzania itaendelea kukopa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo reli ya kisasa.

Kauli ya Msama imekuja kukiwa na mjadala mkubwa huku baadhi ya wanaCCM wakiwemo viongozi wa mikoa na jumuiya wa chama hicho, wakimpinga Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu kauli yake kutounga mkono uamuzi Serikali wa kukopa.

Desemba 28 mwaka huu, akiwa mkoani Dodoma katika mkutano wa pili wa wanakikundi cha Mkalile Ye Wanyusi Spika Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge wa kuanzisha na kupitisha tozo za miamala ya simu kuliko kuendelea kukopa.


Siku iliyofuata katika utiaji wa saini wa mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa wa SGR uliofanyika Ikulu Dar es Salaam, Rais Samia alisema Serikali itaendelea kukopa ili kukamilisha ujenzi wa reli hiyo  kwa awamu nyingine.

Lakini juzi, Msama amewaambia wanahabari kuwa Rais Samia anapaswa kuungwa mkono na kupongezwa akisema mikopo ambayo nchi imeichukua na itakayoichukua kwa siku za usoni itakuwa kwa maslahi ya kila Mtanzania.

"Ni vigumu kufanya maendeleo makubwa bila kukopa, namuomba Rais Samia asitishwe wala kuogopa na maneno yanayozunguzwa na baadhi ya watu wasiotakia mema Taifa hili. Mama (Rais Samia), aendelee kuchapa kazi tupo naye bega kwa bega. amesema Msama.

Msama amesema kuna mataifa makubwa yamepiga hatua za maendeleo kutokana na mikopo yenye tija kama ambayo Rais Samia ameridhia Serikali kuichukua. 

"Miradi inayotekelezwa kwa sasa ndani ya nchi ni mikubwa na kwa kodi za ndani haiwezi kukamilika kwa wakati.Rais amechukua hatua ya ujasiri mkubwa kwa manufaa ya Taifa letu," amesema Msama.