Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msichana wa kwanza kitaifa kidato cha nne aeleza matarajio yake

Msichana wa kwanza kitaifa kidato cha nne aeleza matarajio yake

Muktasari:

  • Justina Gerald (15) mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Canossa aliyeshika nafasi ya kwanza kwa wasichana katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2020 amesema anataka kuwa mhandisi wa mafuta.

Dar es Salaam. Justina Gerald (15) mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Canossa aliyeshika nafasi ya kwanza kwa wasichana katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2020 amesema anataka kuwa mhandisi wa mafuta.

Mbali na kuwa wa kwanza kwa wasichana katika mtihani huo, Justine aliyesema siri ya kufaulu ni kumtanguliza Mungu katika masomo,  ameshika nafasi ya pili katika orodha ya wanafunzi 10 bora kitaifa.

 “Kwanza ni kumtanguliza Mungu kwa kila jambo, pia ni kuweka nia na malengo na kuhakikisha nayatekeleza na pia kushirikiana na wanafunzi wenzangu na walimu na wazazi,” amesema Justina alipozungumza na Mwananchi Digital.

Kuhusu matarajio yake amesema anataka kuwa mhandisi wa mafuta na ndio kozi  anayotamani kuisoma atakapojiunga chuo kikuu.

 “Nataka kuwa mhandisi wa mafuta ya petroli kwa sababu nchi zinazoendelea kama Tanzania ndiyo zinategemea kukuza uchumi wake,” amesema Justina.