Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtafiti Rugalema: Ulaji mbogamboga na maharage uko chini

Muktasari:

  • Wakati ulaji wa mbogamboga na maharage Afrika ukiwa bado uko chini, uwekezaji katika mbegu bora, uwezeshaji na kujenga utamaduni wa ulaji vitu hivyo kwa watoto imetajwa kuwa moja ya njia inayoweza kuchochea.

Dar es Salaam. Wakati ulaji wa mbogamboga na maharage Afrika ukiwa bado uko chini, imeelezwa kuwa uwekezaji katika mbegu bora, uwezeshaji na kujenga utamaduni wa ulaji wa bidhaa hizo kwa watoto, ni njia inayoweza kuchochea mabadiliko.

Dhana hio inatokana na kile kilichoelezwa kuwa, kwa kawaida mtu hutakiwa kula gramu 400 za mbogamboga kwa siku, hata hivyo tafiti zinaonyesha matumizi ni gramu 100 pekee; huku kwenye ulaji wa maharage ukiwa ni gramu 65, kinyume gramu 100 zinazopendekezwa.

Mambo haya yameelezwa jana Septemba 5, 2023; katika mkutano wa kando, ulioandaliwa kwa ajili ya kujadili umuhimu wa mbogamboga na maharage katika kujenga lishe, kama sehemu ya mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika 2023 (AGRF), ulioanza Septemba 5 jijini hapa.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Kimataifa ya Mazao ya Mbogamboga, Dk Gabriel Rugalema, amesema mboga na maharage ni chakula na lishe ambacho husaidia kuzuia magonjwa nyemelezi lakini ulaji wake bado ni wa kusuasua.

Amesema kwa sababu ulaji wake ni mdogo ni vyema Serikali ikaangalia namna ya kubadilisha sera ili ziweze kulenga mazao hayo moja kwa moja hasa katika uendelezaji wa mbegu zake, ulaji na kuweka uwezeshaji ili mazao hayo yawe katika mfumo wa chakula

"Mfano shuleni watoto wale chakula chenye mboga na maharage kwa sababu ni muhimu kwa afya yao hasa katika umri balehe, pia wakulima waelimishwe na kuwekewa mazingira wezeshi pamoja na sera," amesema Dk Rugalema.

Katika upande wa uzalishaji, Gloria Phekani kutoka Milele Agroprocessing Limited ya Malawi, amesema hayo yote yatafanikiwa ikiwa wakulima wataeleweshwa, na kupewa taarifa toshelezi juu ya mbegu wanazotakiwa kutumia ili waweze kujiinua kimaisha.

"Serikali zianze kuona kilimo kama biashara na Serikali ziingie huko kwa hali ya juu na si kuja kuangalia tu watu wamefanya nini, pia wawaelekeze wakulima nini cha kufanya," alisema amesema Gloria.

Pia wakulima wapewe mbegu bora kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zao katika kisi kinachotakiwa.

Suala la mbegu bora liliungwa mkono na Mwanasayansi kutoka World Vegetable Center, Dk Sognigbe N'Danikou amesema Afrika inatakiwa kuwekeza katika uzalishaji wa mbegu tunazohitajika.

Mbegi hizo pia ziwe ndiyo zinazohitajika katoka mnyororo wa thamani ya mazao hayo kuanzia kwa wadau wa mbegu, wakulima hadi walaji.

"Wakati haya yote yakifanyika lazima tukumbuke kuna changamoto ya mabadiliko ya batianchi na upungufu wa lishe ndani ya Afrika, tukae kwa pamoja kutoka sekta binafsi na za umma kuangalia nini tunaweza kufanya kutatua changamoto hizi," amesema N'Danikou.

Alisema hilo pia linaweza kuchangia kufanya mazao hayo kuwa ya kibiashara yana fursa kubwa ya soko ambalo vijana wanaweza kulitumia.

"Hili litafanikiwa ikiwa vijana wanaofanya kazi katika sehemu hiyo watasaidiwa kikamilifu," amesema N'Danikou.