Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua yaezua madarasa wanafunzi wakiwa darasani

Muktasari:

  • Mvua iliyoambatana na upepo imeleta maafa katika mikoa ya Lindi na Mtwara, yabomoa madarasa na kusababisha kufungwa kwa daraja linalotenganisha wilaya za Masasi na Ruangwa

Mtwara/Lindi.  Mvua na upepo mkali umelata madhara katika mikoa ya Lindi na Mtwara, ikiwamo  kuezua paa la madarasa mawili ya Shule ya Msingi Litehu na kubomoka wakati wanafunzi wakiwa darasani.

Pia mvua hizo zimeleta madhara katika manispaa ya Lindi ambapo nyumba mbili zimeangukiwa na minazi, moja ikiwa na mtoto ndani.

Akizungumzia tukio la kubomoka kwa darasa, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Patrick Sawala amesema hakuna kifo chochote kilichotokeza zaidi ya madarasa mawili na ofisi ya walimu kuezuliwa paa na kubomoka.

Amesema wakati tukio hilo linatokea baadhi ya wanafunzi walikuwa darasani wakiendelea na masomo, ambapo baada ya upepo kuezua paa ukuta ulidondoka.

 “Hakuna maafa yaliyojitokeza ila wanafunzi 20 walipata mshtuko na watano walipata michubuko ambapo walipata huduma na kurejea nyumbani, jitihada zimefanyika na watoto wataendelea na masomo,” amesema Kanali Sawala.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amewataka wananchi mkoani humo kuchukua tahadhari dhidi ya mvua hizo kuepusha madhara.

“Muhimu kuchukua tahadhari tena kwa umakini zaidi hasa kipindi hiki cha mvua, kwa sababu zikiacha kuleta uhabarifu zinaweza kuleta magonjwa ya milipuko.

“Magonjwa mengi ni rafiki na hali hii ya hewa ni vema tukatoa taarifa tunapoona viashiria vyovyote kwa kamati za maafa ziweze kushughulikia,” amesema Kanali Abbas.

Hali hiyo imejitokeza pia mkoani Lindi kwa nyumba mbili zimeangukiwa na minazi katika kata ya Nangaru.

Diwani wa Nangaru, Salumu Ng'ondo amesema,"hakuna mtu aliyepata madhara zaidi ya nyumba kuharibika katika kijiji cha Mkomba Mosi na tukio lingine limetokea kitongoji cha Uleka, Mnazi uliangukia kwenye nyumba ndani kulikuwa na mtoto mdogo aliangukiwa na udongo, akaokolewa na kupelekwa zahanati na alipofanyiwa  uchunguzi alioneka hakupata madhara,” amesema Ng'ondo.

Mvua hizo zimesababisha kufurika kwa mto Rukuredi unaotenganisha Wilaya za Ruangwa na Masasi na kukatisha mawasiliano.