Mwakilishi Jimbo la Mtambwe afariki dunia
Zanzibar. Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe Pemba, Habib Mohammed Ali (ACT-Wazalendo) amefariki dunia.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma wa Chama Cha ACT Wazalendo, Salim Bimani amesema Habib amefariki dunia leo Machi 3, 2023 saa 10:30 alfajiri katika Hospitali ya Saifee jijini Dar es Salaam.
"Chama cha ACT kinatuma Salamu za pole kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, wananchi wa Jimbo la Mtambwe, ndugu jamaa na marafiki wote wa marehemu kwa kuondokewa na kiongozi wetu, mwana familia wetu na mpendwa wetu," amesema.
Bimani amesema taarifa zaidi kuhusu mazishi zitatolewa baadaye baada ya kikao cha familia.
Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake kwa habari zaidi.