Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwana FA ajiingiza kwenye biashara ya manukato

Muktasari:

Unaweza kusema wanamuziki sasa wameamua kusaka fedha mbali na muziki na safari hii Mwana FA naye ameungana na wenzake baada ya kutangaza kuingiza sokoni manukato yake yaitwayo FYN


Mwanamuziki Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA ametangaza kuingiza sokoni manukato yake yaitwayo FYN kuanzia wiki ijayo.

Staa huyo anayetamba na wimbo Hata Sielewi anasema ameona kuna haja ya kuanzisha biashara hiyo ili watu wanukie vizuri.

“Nimeona na sisi tunukie tu vizuri kwani kitu gani bwana! Waungwana, ndugu zangu wapendwa, body sprays (manukato) zitakuwa sokoni kuanzia wiki ijayo,”ameandika msanii huyo katika ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na picha za manukato hayo.

Kwa hatua hiyo Mwana Fa anaendelea kuongeza idadi ya wasanii wenye bidhaa zao sokoni kwani jana, supastaa Vanessa Mdee naye alizindua viatu kwa ajili ya wanafunzi.

Wengine ambao tayari wana bidhaa zao sokoni ni Jux, Alikiba, Wema Sepetu, Diamond, Aunty Ezekiel na Riyama.