Mwanaume auliwa na mume wa anayedaiwa kuwa mpenzi wake

Muktasari:
- Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Kibwana Musa mkazi wa Kijiji cha Kiziwa Kata ya kiroka wilayani Morogoro, amekutwa ameuawa alfajili ya kuamkia leo Juni 22,2022 kwa kukatwa panga nyumbani kwa mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake.
Morogoro. Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Kibwana Musa mkazi wa Kijiji cha Kiziwa Kata ya kiroka wilayani Morogoro, amekutwa ameuawa alfajili ya kuamkia leo Juni 22, 2022 kwa kukatwa panga nyumbani kwa mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mbena Loki amesema Musa aliuawa na mtu aliyedaiwa kuwa ni mume wa mwanamke huyo aliyemtaja kwa jina la Farida Ally.
Mwenyekiti huyo amesema taarifa za kuuawa kwa mwanaume huyo zilianza kusambaa asubuhi na uongozi wa Kijiji ulifika eneo la tukio na kumkamata mwanamke huyo na kumpeleka kituo kidogo cha Polisi Mkuyuni kwa ajili ya usalama wake.
“Taarifa nilizonazo ni kwamba, kwa muda mrefu huyo mwanamke aliachana na mume wake (ambaye ni mtuhumiwa), hivyo alianzisha uhusiano wa mapenzi na marehemu, hata hivyo, mtuhumiwa alikuwa akiendelea kumfuatilia huyu mwanamke," amesema Loki.
“Leo kaamua kumvizia na kumkuta ndani na kuamua kumuua mwanaume mwenzake kwa kumkata mapanga," alisema.
Mtuhumiwa baada ya kufanya mauaji hayo alikimbia na jitihada za kumsaka zinaendelea.
Mwananchi inafatilia zaidi tukio hilo.