Mwenyekiti CCM Kilosa atoa ahadi kwa viongozi, wanachama

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilosa, Amer Mbaraka Ahmed akifurahi mara baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo . Picha Hamida Shariff, Morogoro

Muktasari:

Mwenyekiti mteule wa CCM Wilaya ya Kilosa, Amer Mbaraka ameahidi kusimamia utekelezwaji wa miradi ya maendeleo.

Kilosa. Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Uenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilosa, Amer Mbaraka ameahidi kusimamia utekelezwaji wa miradi ya maendeleo katika eneo hilo.

Hii ni mara ya pili Mbaraka anatwaa wadhifa huo ndani ya Wilaya ya Kilosa, amepata kura 1,212 dhidi ya 341 za mpinzani wake Michael Mkolokoti.

Katika mazungumzo yake baada ya ushindi huo leo, Oktoba 3, 2022 Mbaraka amesema: "Nawaahidi sitawaangusha wajumbe na chama changu”.

Ameelekeza kuvunjwa makundi yaliyokuwepo kabla ya uchaguzi ndani ya chama hicho na badala yake wanachama wote wanapaswa kumuunga mkono ili kukiimarisha chama hicho.