Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwili wa Askofu Kwangu uliokutwa ukielea ziwani kuzikwa kesho

Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu

Muktasari:

Mwili wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu unatarajiwa kupumzishwa kesho Jumatatu Desemba 5, 2022 katika makaburi yaliyopo kwenye dayosisi hiyo mjini Kati mkoani Mwanza.

Mwanza. Mwili wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu unatarajiwa kupumzishwa kesho Jumatatu Desemba 5, 2022 katika makaburi yaliyopo kwenye dayosisi hiyo mjini Kati mkoani Mwanza.

Mwili huo ulitoweka tangu Novemba28, ulikutwa kukutwa Desemba 1, 2022 ukielea juu ya maji Ziwa Victoria karibu na eneo linapojengwa daraja la JPM maarufu kama Kigongo-Busisi Wilaya ya Misungwi mkoani humo.

Akizungumza kwa niaba ya familia jana Jumamosi, Desemba 3, 2022 na Mwananchi Digital kwa simu, Mchungaji Allan Kwilasa alisema wamepewa uhuru na jeshi la polisi kuamua siku ya kumpumzisha mpendwa wao na wao kama familia kuamua kumpumzisha siku ya Jumatatu.

Alisema misa ya mazishi itafanyika Dayosisi ya Victoria Nyanza pamoja na kumpumzisha askofu huyo mstaafu kwenye makaburi ya dayosisi hiyo akidai baada ya mazishi ndio mambo mengine yataendelea.

“Mambo mengine yataendelea baada ya mazishi lakini kwa sasa tumeshakabidhiwa mwili na upo Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando,”alisema Kwilasa

Balozi wa eneo la Butindo yalipo makazi ya marehemu Boniface, Elias Kasigara alisema amesikitishwa na taarifa za kifo cha mkazi huyo wa eneo lake akidai hakuwa na muda mrefu tangu ahamie eneo hilo.

“Kwa kipindi kifupi tangu ahamie hapa alikuwa ni mtu ambaye tulikuwa tunashirikiana katika shughuli za kijamii, hakika alikuwa ni mtu anayethamini maendeleo ya Butindo,” alisema

kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi bado uchunguzi wa kifo cha marehemu Boniface unaendelea na utakapokamilika jeshi hilo litatoa taarifa.