Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni kivumbi uchukuaji fomu uenyekiti CCM Mbeya

Katibu Mwenezi wa CCM ,Mkoa wa Mbeya Christopher Uhagile akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na idadi ya makada waliochukua fomu kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Waliochukua fomu CCM Mbeya wafikia 30, Kaimu Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, Clemens Mponzi ameliambia Mwananchi leo Jumanne Novemba 14, 2023.

Mbeya. Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kimesema idadi ya waliochukua fomu ya kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mbeya, wamefikia 30.

Akizungumza na Mwananchi Digital, leo Jumanne Novemba 14,2023 Kaimu Katibu wa CCM Mkoa, Clemens Mponzi amesema kuwa idadi hiyo imeongezeka kutoka 23 waliochukua Novemba 11 na 12 mwaka huu.

“Tunaona kasi ipo kama chama kinaendelea kuhamasisha wanachama kujitokeza kuchukua fomu sambamba na wanawake wasiwe nyuma kwani wanayo fursa ya kuwa viongozi ndani ya chama,” amesema.

Alipohojiwa kuhusiana na ushiriki wa wanawake kwenye kujitokeza kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama hicho mkoani humo, amesema hawako nyuma na kwamba wanajitokeza kuwania huku akisema chama kinahitaji wagombea wengi zaidi.

Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa CCM mkoani humo, Christopher Uhagile amesema kuwa mwamko ni mkubwa kwani bado zoezi la utoaji wa fomu bure linaendelea huku akisisitiza watia nia kutoanza kampeni kabla ya wakati.

“Nitumie fursa hii kutaka wanaCCM kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo na  kurudisha kwa wakati  ili kuanza vikao vya kupitisha majina kwa ajili ya kuanza kampeni rasmi za kuomba kura kwa wajumbe.” amesema .

Amesema Rai yake ni kuona idadi kubwa ya wanachama wanaochukua fomu ili kuonyesha ukomavu wa chama katika kutekeleza demokrasia huru ya kuomba ridhaa ya uongozi.

Miongoni mwa waliochukua fomu leo Jumanne Novemba 14,2023 ni  pamoja na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa cham ahicho (Uvccm) Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna, na aliyekuwa  Mwenyekiti wa Halmashari ya Wilaya ya Kyela mkoani hapa Hunter Mwakifuna .