Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

OCD Simanjiro ataka manaofuja fedha za umma wakamatwe

Mkuu wa Polisi (OCD) wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mathayo Mmary ambaye ni mgeni rasmi kwenye mkutano wa nusu mwaka wa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii akizungumza na viongozi wa vyombo hivyo vilivyo chini ya wakala wa maji na usafi wa mazingira (Ruwasa). Picha na Joseph Lyimo

Simanijro. Mkuu wa Polisi Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mathayo Mmary amesema watumishi wa Serikali wanaofuja fedha za umma wanapaswa kukamatwa na siyo kuhamishwa eneo lingine.

Mmary amesema hayo LEO Jumapili Aprili 23, 20232 wakati akifungua mkutano wa nusu mwaka wa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Dk Suleiman Serera.

Amesema mtumishi wa Serikali anapofanya makosa ya kufuja fedha za umma anapaswa kuchukuliwa hatua kali, ikiwemo kufikishwa polisi kisha mahakamani ili iwe funzo kwake. “Wanaokula fedha za umma wasihamishwe kutoka eneo moja kwenda lingine kwani wataendelea kufuja fedha walipohamia, dawa ni kuwashtaki mahakamani ili waende jela,” amesema.

Amesema mtindo wa kuwahamisha watumishi wanaofuja fedha za umma kutoka eneo moja hadi jingine ni kufuga maradhi hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kukomesha.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (Ruwasa) wilaya ya Simanjiro, Joanes Martin amesema hadi hivi sasa vijiji 44 vinapata maji kati ya vijiji 68 na wanatarajia kuongeza vijiji vingine 12.

Mhandisi Martin amesema upatikanaji wa maji wilayani hapo ni asilimia 58 ambapo wananchi 178,000 wanapata maji na wanatarajia hadi mwezi Desemba itakuwa asilimia 63.

Mwenyekiti wa chombo cha watoa huduma ya maji ngazi ya jamii kata ya Ngorika, Patrick Mbogo amesema kila siku wazee 25 wanapatiwa maji ndoo mbili bila kulipia, "Pia tumejiwekea utaratibu wa kutoa uniti mbili sawa na ndoo 100 za maji bila malipo pindi ukitokea msiba kwenye eneo hili," amesema Mbogo.