Padri kortini akidaiwa kudhalilisha watoto kingono

Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, Sostenes Soka (aliyejifunika uso kwa koti) akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za udhalilishaji wa kingono kwa watoto.

Muktasari:

  • Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, Sostenes Bahati Soka amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za udhalilishaji wa kingono kwa watoto.

Moshi. Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, Sostenes Bahati Soka amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za udhalilishaji wa kingono kwa watoto.

Kiongozi huyo wa kiroho, amepandishwa leo Jumatatu, Septemba 26, 2022 kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha.

Hata hivyo, waandishi wa habari wamezuiwa kuingia katika chumba cha mahakama kwa kile kilichoelezwa ni aina ya kesi inayomkabili padri huyo.

Hakimu huyo amewaeleza waandishi wa habari kuwa atazungumza nao baadaye.

                                             

Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa habari zaidi