Polisi auawa kwa kukatwa panga

Polisi auawa kwa kukatwa panga

Muktasari:

  • Askari polisi katika kituo kidogo cha polisi Mbughuni, PC Damas ameuawa kwa kukatwa na panga kichwani wakati akijaribu kumkamata mtuhumiwa.wa wizi.

Arusha. Askari polisi katika kituo kidogo cha polisi Mbughuni, PC Damas ameuawa kwa kukatwa na panga kichwani wakati akijaribu kumkamata mtuhumiwa.wa wizi.

Kufatilia mauaji hayo kikosi cha polisi kikiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha , Jastine Masejo kinaendelea na operesheni kumsaka mtuhumiwa.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa tano usiku katika Kijiji cha Makiba wakati askari huyo alipoenda nyumbani kwa mhalifu kwa lengo la kumkamata .

Kwa mujibu Kamanda wa Masejo askari huyo alifariki dunia muda mfupi baada ya kuvunja damu nyingi.

“Askari wetu katika kituo kidogo cha polisi Mbughuni alikatwa panga kichwani na kufariki dunia baada ya kwenda nyumbani kwa mhalifu majira ya saa tano usiku lengo la kumkamata, hivi sasa polisi wanaoendesha operesheni ya kumsaka ili afikishwe kwenye vyombo vya dola,” amesema.

Amesema wakati wa harakati za kumkamata ndipo alipotokea mhalifu mwingine nyumba ya jirani ambaye alimkata panga moja kichwani askari huyo na kupoteza naisha.