Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Nachingwea yajipanga kukabiliana na uhalifu, ukatili wa kijinsia

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi wilayani Nachingwea limeandaa mpango wa kupambana na wizi na ukatili wa kijinsia majumbani kwa kuunda kamati za ulinzi shirikishi itakayokuwa na jukumu la kuwabaini na kuripoti matukio hayo ili hatua zichukuliwe haraka.

Nachingwea. Jeshi la Polisi wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi limeandaa mpango maalumu wa kupambana na vitendo vya uhalifu na ukatili wa kijinsia vilivyokithiri kwenye baadhi ya vijiji wilayani humo.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo, Aprili 21, 2024, Mkaguzi wa Polisi Kata ya Mtua wilayani humo, Frank Mwanisi amesema kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo, Jeshi la Polisi limeanza kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi kwa lengo la kupambana navyo na kutoa elimu juu ya matukio hayo ya ukiukwaji wa sheria.

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema, tumeamua kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi, ili kutokomeza kabisa vitendo vya wizi na ukatili ambao mara nyingi wamekuwa wakifanyiwa wanawake na watoto katika baadhi ya vijiji wilayani hapa,” amesema Mwanisi.

Mwanisi amefafanua kuwa baada ya kuundwa kwa vikundi, hivyo watakuwa wanawapatia elimu wananchi ili kukabiliana na vitendo hivyo ili kuwa na vijiji vyenye amani.

“Vikundi hivi vitasaidia kupunguza wizi na tunatoa elimu ya ukatili wa kijinsia katika kila kijiji ili jamii iachane na tabia hizo, ambazo hazina tija kwa Taifa,” amesema.

Bakari Juma, mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea amesema Jeshi la Polisi likijitahidi kuunda vikundi vingi kila vijiji itasaidia kuondoa matukio hayo mabaya kwa jamii zetu

“Uundaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi vitasaidia kuondoa uhalifu kwa sababu wataogopa kufanya uhalifu kwa kujua kwamba kuna ulinzi na muda wote wapo macho,” amesema Bakari.

Naye Stella Peter, amesema baadhi ya watu katika maeneo tofauti ya Nachingwea wamekuwa wakitishia watu na akuwafanya waishi kwa hofu.

“Jeshi la Polisi lijitahidi kuunda vikundi haraka kila kijiji ili kutokomeza uhalifu unaojitokeza mara kwa mara kwenye maeneo yetu,” amesema Stella.