Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi wakamata bidhaa feki za tani 12 Zanzibar

Muktasari:

Bidhaa zilizokamatwa na polisi kwa kushirikiana na ZFDB ni unga, mchele na pampasi.


Zanzibar. Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Bodi ya Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) wamekamata tani 12 za mchele, unga na pampasi zilizokwisha muda wa matumizi katika ghala lililopo eneo la Migombani, Unguja.

Kamishna msaidizi wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Thobias Sedoyeka na mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud ndio waliongoza ukamataji huo leo Jumatano Mei 30, 2018.

Sedokeya amemtaja mmiliki wa bidhaa hizo kuwa ni mfanyabiashara, Mohamed Matar na kumtaka ajisalimishe haraka polisi, kubainisha kuwa hawawezi kuvumilia wananchi kuuziwa na kugawiwa vyakula vilivyomaliza muda wake.

Amesema baada ya hatua hiyo, wataanza msako wa nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kuwabaini walioficha vyakula.

Akizungumza na MCL Digital kaimu mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Dk Khamis Ali amewaka wananchi kutoa ushirikiano wa kina kwa mamlaka hiyo ili kuwanusuru wananchi kutolishwa vyakula vibovu.