Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi yamshikilia mlinzi anayedaiwa kuua mwananchi kwa risasi

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mlinzi wa Hospitali ya Challote inayomilikiwa na Masista wa Kanisa Katoliki Wilaya ya Siha kwa madai ya kumuua kwa risasi mkazi wa Kitongoji cha Kilari, wilayani humo, Nicholous Nzota.

Siha. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mlinzi anayelinda shamba la Masista wa kanisa Katoliki ambalo lipo jirani na hospitali ya Challote Wilaya ya Siha kwa madai ya kumuua kwa risasi mkazi wa Kitongoji cha Kilari, wilayani humo Nicholous Nzota (35-40).

Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk Christopher Timbuka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lilotokea saa moja usiku, Oktoba 1, 2023 katika eneo la hospitali hiyo huku akisema chanzo ni baada ya walinzi hao kuwashikilia mateka wanawake wawili waliowakuta mpakani wa eneo la hospitali hiyo jambo ambalo lilileta vurugu baina ya wananchi na walinzi hao.

"Ni kweli jana saa moja usiku kulitokea tukio la mauaji katika Kitongoji cha Kilari, kuna bwana mmoja alipigwa risasi na mlinzi wa Hospitali ya Challote ambapo chanzo ni ugomvi uliotokea baada ya walinzi kuwashikilia mateka wanawake wawili waliokutwa mpakani mwa eneo la hospitali," amesema Dk Timbuka.

Alipotafutwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo, amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mlinzi huyo kwa mahojiano zaidi juu ya tukio hilo.

"Jeshi la Polisi tunamshikilia mlinzi wa hospitali hiyo, tunaendelea na jitihada za uchunguzi zaidi juu ya tukio hili la mauaji," amesema Kamanda Mdogo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kwa taratibu nyingine zaidi.