Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Profesa Kitila amzungumzia mrithi wa Kinana CCM

Muktasari:

Asema kwa zama za sasa ni mtu sahihi kabisa


Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Bashiru Ally ni mtu sahihi kwa zama za sasa kuwa katibu mkuu wa chama hicho tawala.

Jana Halmashauri Kuu, ambayo ni chombo cha pili kwa ukubwa cha CCM ilikutana kwa siku mbili Ikulu jijini Dar es Salaam, na kumpitisha msomi huyo ambaye aliongoza kamati iliyohakiki mali za chama hicho kwa miezi mitano, kuwa katibu mkuu.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter Profesa Mkumbo amesema, “katika kipindi ambacho silaha ya siasa ni nguvu ya hoja, weledi, na uimara CCM imepata katibu mkuu sahihi kwa zama sahihi nakutakia mafanikio makubwa komredi Dk Bashiru Ally.”

Uteuzi huo umekuja baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kuandika barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.