Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Lungu: Magufuli ameunyanyua uchumi wa Zambia

Rais Lungu: Magufuli ameunyanyua uchumi wa Zambia

Muktasari:

  • Rais wa Zambia Edgar Lungu ameelezea kuumizwa na kifo cha rafiki yake Hayati Rais John Magufuli huku akielezea namna alivyolinyanyua Taifa la Zambia kiuchumi kupitia reli ya  Tazara.

Dar es Salaam. Rais wa Zambia Edgar Lungu ameelezea kuumizwa na kifo cha rafiki yake Hayati Rais John Magufuli huku akielezea namna alivyolinyanyua Taifa la Zambia kiuchumi kupitia reli ya  Tazara.

Lungu ameyasema hayo leo Machi Jumatatu Machi 22, 2021 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakati wa kuaga mwili wa Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena alikokuwa akipatiwa matibabu.

Amemwombea kiongozi huyo apumzike kwa amani huku akimtaja kuwa ni mwana wa Afrika aliyepigana vita vilivyo vyema.

“Ameacha alama nchini Tanzania kwa moyo wake wa kujitolea atakumbukwa kwa mchango wake katika jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika (Sadc) hasa baada ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya yetu.”

“Kwa upande wetu kama Zambia uchumi wetu umeimarishwa zaidi kupitia reli tumeweza kufanya miradi ya pamoja kama Tazara na bomba la mafuta, Novemba 2016 nilipokutana naye tulionyesha tena nia yetu ya kuimarisha miradi yetu kwa faida yetu wote,” amesema Lungu.

Amesema Oktoba 2019 walizindua kituo cha huduma za pamoja, “Ninalokumbuka ni moyo wake wa kuhamasisha watu alipoongea nao watu wa mpaka wa Tanzania na Zambia alikuwa aliyenyooka na mwanamageuzi.

Kwangu binafsi si tu alikuwa mwanamageuzi alikuwa rafiki yangu wa karibu nitamkosa sana. Magufuli alikuwa rafiki yangu sana na hii imeniuma sana sana, naomba Mungu amuweke mahali pema peponi Amen.”