Rais Mwinyi avunja bodi Zanzibar

Muktasari:
- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameivunja bodi ya ushauri ya kudhibiti vileo Zanzibar.
Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameivunja bodi ya ushauri ya kudhibiti vileo Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imesema hatua hiyo ni kuanzia leo Jumanne Septemba 7, 2021.
Bodi hiyo ilikuwa chini ya usimamizi wa Ofisi Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ.
Pia, Rais Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS), Rahima Ali Bakari.