Rais Nkurunziza, Trump walivyokuwa mada ya dunia

Rais Nkurunziza, Trump walivyokuwa mada ya dunia

Muktasari:

Pierre Nkurunziza, Rais wa pili wa Burundi alikuwa gumzo la dunia alipojitengenezea mazingira ya kuwa kiongozi mkuu baada ya kuachia madaraka.

Pierre Nkurunziza, Rais wa pili wa Burundi alikuwa gumzo la dunia alipojitengenezea mazingira ya kuwa kiongozi mkuu baada ya kuachia madaraka.

Kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 20, Katiba ya Burundi ilibadilishwa kumwezesha Nkurunziza kuwa mwelekezi mkuu wa Rais wa Burundi hata baada ya kuchia ngazi lakini alifariki Juni 8, siku 19 baada ya uchaguzi mkuu na miezi miwili hajakabidhi kijiti kwa mrithi wake, Evariste Ndayishimiye.

Kifo cha Nkurunziza kiligeuka gumzo la ulimwengu kwani kilikuwa cha ghafla. Wakati Nkurunziza anafikwa na mauti, mkewe, Denise Bacumi-Nkurunziza, alikuwa kwenye matibabu ya corona jijini Nairobi, Kenya.

Rais Nkurunziza, Trump walivyokuwa mada ya dunia

Desemba 17, Burundi ilitikisa vichwa vya habari duniani baada ya Rais wake wa zamani, Pierre Buyoya kufariki akiwa Ufaransa kutokana na maradhi ya corona.

Buyoya aliiongoza Burundi kati ya mwaka 1987 na 1993 aliposhindwa uchaguzi wa kidemokrasia akigombea kupitia chama cha Uprona. Alishindwa na Melchior Ndadaye wa chama cha Frodebu. Buyoya aliiongoza tena Burundi kati ya mwaka 1996 hadi 2003.

Afrika Kusini

Anapotajwa Nelson Mandela, Rais wa kwanza wa Afrika Kusini kumbukumbu za kifo cha binti yake, Zindziswa Mandela, aliyefariki Julai 13 kutokana na corona, hazifutiki.

Wakati anafariki Zindziswa alikuwa amemaliza utumishi kama balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark na alikuwa anasubiri kwenda Liberia kwa nafasi hiyohiyo.

Zindziswa, mtoto wa Winnie Mandela, ndiye aliyesoma tamko la Mandela la mwaka 1985 kupinga masharti ya Serikali ya ubaguzi wa rangi, lililomtaka aachiwe gerezani lakini asijishughulishe tena na siasa.

Julai 21, Andrew Mlangeni, mfungwa pekee aliyebaki kati ya wafungwa wa kesi maarufu Afrika Kusini, Rivonia Trial, alifariki dunia. Kesi hiyo ndiyo ilimpeleka jela maisha Mandela na wenzake ingawa wote waliachiwa baada ya kutumikia kati ya miaka 25 mpaka 27.

Rais Nkurunziza, Trump walivyokuwa mada ya dunia


Ethiopia

Kifo cha Hachalu Hundesa, mwanamuziki na mwanaharakati wa Ethiopia, aliyeuawa kwa kupigwa risasi Juni 29, kilitikisa na kuibua maandamano. Watu wakisema Serikali ilihusika.

Rais Nkurunziza, Trump walivyokuwa mada ya dunia

Hachalu alikuwa sauti ya Waoromo na ndio sababu mamilioni waliingia barabarani kudai haki. Kifo hicho kilisababisha vingine vingi vya waandamanaji walioharibu mnara wa Haile Selassie. Mpaka sasa viongozi wa Oromo wapo mahabusu kutokana na ghasia za kifo cha Hachalu.

Kabla la Hachalu halijaisha, ukaibuka mgogoro wa Tigray. Eneo la Kaskazini ya Ethiopia, kupitia serikali yake, ilipinga kuendelea kukaa madarakani kwa Abiy. Kwamba hakuwa halali baada ya kuahirisha uchaguzi kwa sababu ya corona.


Mali

Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, alipinduliwa Agosti 19 baada ya maandamano ya wananchi ya muda mrefu.

Keita alishutumiwa kwa kushindwa kumaliza vurugu za vikundi vya kigaidi, kukomesha utekaji na upotevu wa watu hata kuimarisha uchumi.

Mara kadhaa Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas), zilijaribu kutuliza maandamano yaliyokuwa yanaendelea bila mafanikio yoyote.

Rais Nkurunziza, Trump walivyokuwa mada ya dunia


Brazil

Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro ni miongoni mwa viongozi ambao habari zao zilitamba sana mwaka huu. Corona ilipoingia Brazil, Bolsonaro alipuuzia, akasema ni ugonjwa wa vyombo vya habari.

Rais huyo hakujali chochote kuhusu corona na akasema hawezi kutishwa na ‘vimafua.’ Mwisho, Bolsonaro aliugua corona.

Rais Nkurunziza, Trump walivyokuwa mada ya dunia

Marekani

Rais Donald Trump wa Marekani, ametawala vyombo vya habari duniani kwa kiasi kikubwa. Trump alipata maambukizi ya ugonjwa wa corona, mkewe Millania, na wasaidizi wake wengi, akiwa Ikulu ya Marekani.

Trump amekuwa akigombana na wataalamu wa afya nchini humo kuhusu namna ya kukabiliana nao. Mmoja wa wataalamu ambao alisuguana naye sana ni mkuu wa magonjwa ya kuambukiza, Dk Anthony Fauci.

Trump aliangushwa na Joe Biden, kwenye uchaguzi wa Rais hivyo kumfanya atajwe sana duniani.

Uchaguzi ulifuatiliwa duniani kote hivyo kumnyima ushahidi wa kutosha kuthibitisha kaibiwa kura.

Rais Nkurunziza, Trump walivyokuwa mada ya dunia


Makala hii imeandwa na Maloto