Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia atoa pole kifo cha Malkia Elizaberth II

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na kifo cha Malikia Elizaberth II wa nchini Uingereza, kilichotokea jana Alhamisi Septemba 8, 2022 katika visiwa vya Balmoral nchini Scotland alipokuwa anapatiwa matibabu.


Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na kifo cha Malikia Elizaberth II wa nchini Uingereza, kilichotokea jana Alhamisi Septemba 8, 2022 katika visiwa vya Balmoral nchini Scotland alipokuwa anapatiwa matibabu.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ameandika, “Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Malkia Elizabeth II. Kwa niaba ya Watanzania wote, natuma salamu za pole kwa familia ya Kifalme@RoyalFamily na raia wote wa Uingereza. Malkia atakumbukwa duniani kote kama nguzo ya Amani, Umoja na Utulivu.”

Elizaberth II aliezaliwa jijini London April 21, 1926, aliukwa wadhifa wa Malkia akiwa na umri wa miaka 25, mnamo mwaka 1952 baada cha kifo cha baba yake aliyekuwa mfalme wa taifa wa taifa hilo David IV.

Malkia Elizaberth II amefarikii akiwa na umri wa miaka 96, lakini wengi watamkumbuka kwa yale mazuri aliyoyafanya na lile la kuweka rekodi ya kuwa mtawala wa kifalme aliyeongoza kwa muda mrefu mnamo Septemba 9, 2015, na kupita rekodi ya bibi wa bibi yake Malkia Victoria.