RAS Kilimanjaro afariki dunia kwa ajali
Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda amefariki dunia katika ajali eneo la Njiapanda ya KIA, Wilaya ya Hai, akiwa ziarani mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema imetokea saa nane mchana leo Jumanne Juni 18, 2024.
"Ni kweli wakati anatoka KIA amepata ajali mbaya sana, ndio na mimi nakwenda eneo la ajali,"amesema Babu.
Muda mfupi kabla ya ajali hiyo, Nzunda alikuwa na kikao na wadau wa maendeleo kutoka nchini Namibia kilichofanyika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa huo.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi.