Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Songwe aagiza bodaboda wasizuiwe kuingia stendi Tunduma kushusha mizigo

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabir Omary Makame akizungumza na madereva bajaji na bodaboda katika Halmashauri ya mji wa Tunduma.Picha na Denis Sinkonde

Muktasari:

  • Makame amesema kero hiyo imekuwa na urasimu wa matumizi ya stendi kwa makundi ya vijana hususani bodaboda na bajaji, hivyo kuanzia sasa hakuna mtu atakayewazuia kwenda kushusha mizigo ndani ya stendi.

Songwe. Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Omari Makame, ametoa maelekezo kwa watendaji wanaosimamia Stendi ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma iliyopo Mpemba, kuacha kuwazuia waendesha bodaboda na bajaji kuingia kushusha mizigo ya wateja, akisema huduma hiyo inapaswa kutolewa bila urasimu wala ucheleweshaji.

Akizungumza na vijana zaidi ya 1,500 wanaojihusisha na bodaboda na bajaji ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma leo Alhamisi, Julai 9, 2026, Makame amesema Serikali imepokea malalamiko ya vijana wanaolazimika kusubiri ruhusa au kuzuiwa kuingia stendi kushusha mizigo, jambo linalosababisha usumbufu kwao na kwa wateja.

Makame amesema kero hiyo imekuwa na urasimu wa matumizi ya stendi kwa makundi ya vijana hususani bodaboda na bajaji hivyo kuanzia sasa hakuna mtu atakayewazuia kwenda kushusha mzigo ndani ya stendi.

"Tumepokea kero yenu kuanzia sasa mtaingia stendi, mtashusha mzigo na kuondoka bila kucheleweshwa na huduma kwa wananchi ndiyo iwe kipaumbele," amesema Makame.

Makame amewataka watendaji wa halmashauri kuhakikisha mipango ya ujenzi na uboreshaji wa stendi inazingatia mahitaji ya wadau wote wa usafirishaji, ikiwemo kutenga maeneo maalumu ya bodaboda na bajaji ili kurahisisha utoaji wa huduma.

"Lengo la Serikali ni kuweka mazingira rafiki kwa vijana wanaojiajiri katika sekta ya usafirishaji, huku ikiendelea kuboresha huduma kwa wananchi na kuondoa urasimu usio wa lazima," amesema Makame.

Awali, wakiwasilisha malalamiko mmoja wa waendesha bodaboda, Ismail Maiko amesema wakifika stendi kuu ya Tunduma iliyopo Mpemba wanakatazwa kushushia mizigo ndani bila sababu za msingi huku wakihofia kupoteza mizigo ya wateja kwani wanalazimika kushushia nje.

"Tunabeba mizigo mizito, hivyo tukifika hapo wasimamizi wanatuzuia kuingia ndani tunaomba mkuu wa mkoa utusaidie kwani tunapoteza mda kuanza kusubiri wenye mizigo kwani tunaogopa kuipoteza," amesema Ismail.

Samsoni Mzumbwe amesema  Serikali inapaswa kuwapa miongozo wasimamizi wa hiyo stendi kuhakikisha wanawaondolea vikwazo waendesha bodaboda na bajaji ili waanze kushushia mizigo ndani ya stendi.