Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruwasa yakerwa utunzaji wa vyanzo vya maji Tanga

New Content Item (2)

Korogwe. Wakazi wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wametakiwa kusimamia miradi ya maji na kutunza miundombinu ya maji ili kuifanya iwe endelevu.

Wito huo umetolewa na Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa), Wilaya ya Korogwe, mhandisi William Tupa katika mahojiano baada ya mkutano wa wadau wa maji uliofanyika wilaya ya Korogwe kwa ajili kufahamishwa na kuelemishwa juu ya sheria mpya ya maji namba 5 ya mwaka 2019 ambayo inabadili muundo wa usimamizi wa miradi ya maji vijijni.

Mhandisi Tupa amesisitiza kuwa haina maana kujenga miradi hiyo kwa fedha nyingi halafu isitoe maji kama inavyotakiwa.

Kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2023,  mapato ya vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii  yalikuwa Sh188.5 milioni kati ya mapato hayo Sh152.2 milioni ni makusanyo halisi na Sh36.3 milioni ni bakaa ya mwaka uliopita (Julai 2021  - Juni 2022),”amesema.

Naye Ofisa Mendeleo ya Jamii, Ruwasa Mkoa wa Tanga, Hans Mwiiyola amependekeza kuwa kamati na timu ya uendeshaji itenge bajeti ya kutosha ya kufanya upanuzi wa mradi kutokana na sababu kuwa Kuna baadhi ya wateja hawajafikiwa na mtandao wa maji.