Sabaya, wenzake kukata rufaa

Muktasari:

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake watatu wanatarajia kukata rufaa baada ya kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.


Arusha. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake watatu wanatarajia kukata rufaa baada ya kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Sabaya na wenzake wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akitoa hukumu hiyo leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema ameridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka dhidi ya Sabaya na wenzake pasi na shaka.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hukumu hiyo, Wakili wa Sabaya na wenzake Mosses Mahuna amesema hawajaridhika na hukumu hiyo iliyotolewa kwa sababu ina upungufu mwingi