Samia: Nipo tayari kusamehe

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa yuko tayari kuvumilia kukoselewa, kusikiliza ushauri na kusamehe pale anapokosewa ila amewataka wenyeviti wa vyama vya siasa kuongoza vyama vyao kutii sheria.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa yuko tayari kuvumilia kukoselewa, kusikiliza ushauri na kusamehe pale anapokosewa ila amewataka wenyeviti wa vyama vya siasa kuongoza vyama vyao kutii sheria.

Amesema,”Niwaombe wenyeviti wenzangu wa vyama vya siasa tusitazame yaliyopita, tutazame mbele kwa matumaini. Tuweke nguvu katika kujenga Tanzania mpya yenye kusameheana na kuheshimiana.

“Kama mlezi wa amani natakiwa kuwa mvumilivu, msikivu na mwenye kustahimili na niko tayari kufanya hivyo,” Rais Samia Suluhu Hassan

Samia amesema, “Nitasikiliza, nitavumilia mnayoniambia, mnayonikosoa na niko tayari kusamehe pia ili twende vyema lakini mambo haya ni pande mbili niwaombe na wenzangu muwe tayari na kutii sheria.

 “Tuzike tofauti zetu za nyuma na tuendeshe vyema siasa katika nchi yetu, niko tayari kusikiliza wenzangu, najua kuna mengi ya kusikiliza yakiwemo madukuduku, nongwa, hasira na malalamiko yanayotokana na uchanga wetu wa demokrasia,”