Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti hifadhi bora Afrika

Muktasari:

  • Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeshinda tuzo ya Hifadhi Bora Afrika kwa mwaka 2023 ikiwa ni mara ya tano mfululizo, ikizishinda hifadhi shindani kutoka Botswana, Namibia, Uganda, Afrika Kusini na Kenya.

Arusha. Hifadhi ya Taifa Serengeti imeibuka tena kwa mara ya tano kutwaa tuzo ya mshindi wa kwanza wa hifadhi bora barani Afrika kwa mwaka 2023 (Africa’s Leading National Park 2023).

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeshinda kwa tano mfululizo kushinda tuzo hii na miongoni mwa maajabu ya hifadhi hii msafara wa nyumbu wanaohama Kila mwaka na uwepo wa wanyama wengi wanaoonekana kirahisi.

Hifadhi ya Serengeti imetwaa tuzo hiyo baada ya  kuwashinda washindani wa tuzo hii  hifadhi za Central Kalahari Game Reserve- Botwswana,  Etosha National Park -Namibia,  Kidepo Valley National Park -Uganda, Kruger National Park -South Africa, mapoja na Masai Mara National Reserve – Kenya.

Ofisa Mhifadhi Mwandamizi Idara ya Mahusiano, Catherine Mbena amesema tuzo hiyo imetolewa na ‘World Travel Awards’ usiku wa tarehe 15 Oktoba, 2023 katika Hoteli ya  Atlantis The Royal Dubai   katika nchi za Falme za Kiarabu.

Mbena amesema tuzo hiyo imepokelewa na  na Mkuu wa Kanda ya Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Izumbe Msindai, kwa niaba ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).

Katika tuzo hizo pia Hifadhi ya Ngorongoro imeshinda tuzo hizo za hifadhi nzuri kutembelewa barani Afrika.